Kuna magonjwa ya hernia ya aina nyingi kama
zile ziitwazo kitaalamu inguinal, umbilical,
femoral, epigastric, incisional, inguinal hernia
na diaphragmatic hernia.
Lakini watu wengi hukumbwa na hernia
iitwayo inguinal hernia ambayo hutokeza
karibu kabisa na sehemu ya siri ambako hapa
kimrija kinachochukua mbegu za kiume
kutoka kwenye korodani na kuingia kwenye
tumbo na kuingia kwenye kiungo cha kiume.
Hapa panaweza kuwa na uwazi na uwazi huo
ukaingia utumbo mdogo na kusababisha
hernia hii. Aina hii ya hernia kama nilivyosema
hapo juu ndiyo inayosumbua sana watu wengi
duniani.
Kuna aina nyingine ya hernia inayoweza
kutokea kwenye kitovu, sehemu ambayo
kunakuwa na mshipa unaopitisha damu yenye
chakula na hewa safi ya oksijeni kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni.
Sehemu hiyo mtoto anapozaliwa panaweza
pasijifunge vizuri, hivyo mtoto huyo kupata
hernia hii baadaye kwani utumbo mdogo
huingia katika kijinafasi hicho kisichojifunga
vizuri, hivyo kusababisha uvimbe wa hernia hii.
Lakini tatizo hili ikiwa mtoto amezaliwa na
akaishi zaidi ya miaka miwili bila kujitokeza
tena, basi atakuwa salama kwa sababu kwa
muda huo sehemu hiyo huwa imejifunga
kabisa.
TIBA
Ikitokea sehemu hiyo ikaacha kujifunga kwa
kipindi hicho cha miaka miwili, basi daktari
huamua kumfanyia upasuaji mtoto huyo.
Kwa watu wazima hernia kwenye kitovu
ambayo kitaalamu huitwa umbilical hernia
inaweza ikatokea kwa akina mama wenye
mimba au kwa wale ambao ni wanene kupita
kiasi kwani presha kwenye tumbo inakuwa
kubwa na kufunga sehemu hii ya kitovu
ambayo inawezekana awali ilikuwa wazi.
Hernia nyingine huweza kutokea kwenye
kiungo cha njia ya kumezea chakula
kinapoungana na tumbo. Kama sehemu hii
haikufunga vizuri utumbo unaingia kwenye
kinafasi hicho na kujitokeza kwenye kimfuko
kilichopo kifuani kinachoitwa kitaalamu
diaphragm.
Ndiyo maana hernia hii huitwa diaphragm
hernia.
Hernia nyingine iitwayo femoral hernia
hutokea pale mishipa ya damu iendayo
kwenye mguu inapopita kwenye tumbo na
ikiwa kwenye maungio pana nafasi basi hernia
hii hutokea kwenye paja karibu na kiunoni.
Kuna hernia ingine inayotokea kwenye
chembe ya moyo ambapo misuli inaachia na
kusababisha kingozi cha tumbo na utumbo
kuingia katika sehemu hiyo hivyo kuvimba na
kusababisha hernia.
Tiba za uhakika za hernia ni kufanyiwa
upasuaji kama tulivyofafanua hapo juu.
Chapisha Maoni