1. Leo (jana) kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa
11 jioni tulikuwa ktk ukumbi Wa Julius Nyerere
Conference katika kikao cha Kamati ya Bunge ya
Katiba, Sheria na Utawala tukiwawasilisha
mapendekezo ya Muswada wa Mahakama ya
Kadhi.
Tulikuwa taasisi 11: Baraza Kuu la Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu, Tanzania, Annahar, Basuta,
Tampro, Dumt, Shura ya Maimamu, jumuiya na
taasisi mbalimbali kwa upande mmoja na Bakwata
upande wa pili, Tanganyika Legal Society (TLS) nk
nk. Pia alialikwa Jaji Robert Makaramba na Arcado
Ntagazwa.
2. Maoni ya Jaji Robert Makaramba ni kuwa
Mahakama ya Kadhi ni chombo halali na hakipaswi
kuitwa cha kidini bali ni chombo cha dola,
kigharamiwe na dola, Wakristo wasilalamike
sababu hata mahakama za kawaida zinatumia
sheria za Kikristo ambazo zinatokana na Common
Law.
3. Bakwata wao wameiambia Kamati ya Bunge
kuwa Mahakama ya Kadhi ni mahakama ya kidini
hivyo isigharamiwe na dola bali zijigharamie
zenyewe kama tunavyogharamia ‘’maji ya udhu,’’
‘’mikeka’’ na ‘’umeme,’’ misikitini, pia Mahakama ya
Kadhi hiyo ndiyo hii Mufti aliyoiunda, na kwamba
Mufti anayetajwa na muswada awe ni Mufti wa
Bakwata hiyo iwe rasmi ndani ya sheria. Maoni ya
Bakwata yamewasilishwa na Katibu wa Bakwata
Mzee Lolila na Sheikh Hamid Jongo.
4. TLS wao wanapendekeza muswada huu
uondolewe haufai.
5. Maoni yetu ya taasisi 11 kama
yalivyoandaliwa na wanasheria kwa ushirikiano
na masheikh yamewasilishwa na Wakili Njama.
Kimsingi tumesema huu muswada haufai
uondolewe na badala yake kamati tumeiomba
ipokee muswada mbadala tuliouandaa ambao
unaunda Mahakama ya Kadhi, unaunda Bodi ya
Sheria za Kiislam ambayo ndiyo itakayoteua
makadhi na kudhibiti nidhamu za makadhi, pia
Waziri wa Sheria asipewe mamlaka ya kutunga
sheria au kanuni zinazohusu Waislamu bila ya
kushauriana na wanazuoni.
Mahakama ya Kadhi tumetaka iwe sehemu ya
“Judiciary,” igharamiwe na dola. Bakwata na Mufti
wa Bakwata wasiwe ndiyo wateuzi wa makadhi.
Tumeitaka Kamati ya Bunge iishauri serikali
iuondoe muswada wake haufai na wala haukidhi
vigezo vya kuunda chombo chenye hadhi ya
mahakama.
6. Ntagazwa ameeleza historia ya Mahakama ya
Kadhi na ameeleza kuwa muswada huu hauna nia
ya dhati kuanzisha Mahakama ya Kadhi ya ukweli
bali nia ni kupata kura za Waislamu tu. Ntagazwa
aliungana nasi kuwa muswada uondolewe.
7. TLS nao waliunga mkono hoja zetu kwa kiasi
kikubwa. Katika kikao hicho kwa upande wetu
tulikuwa mimi, Wakili Njama, Dr. Benhajj, Wakili
Hamza Jabir, Masheikh: Kundecha, Kilemile, Sheikh
Bawazir, Sheikh Mbalamwezi Mwanahistoria
Mohamed Said na wengi wengine.
Alhamdulillah tuliwakilisha vyema na wrote
walituelewa tunaamini kazi tuliitimiza yaliyobaki
Allah anajua zaidi. Mjadala ulikuwa mkali kutwa
nzima lakini tuliwatuliza.
Aliandika makala Hii ni ndugu ktk Uislam,
Mwanasheria/Wakili Juma N. Dovutwa.
Chapisha Maoni