VIPIMO
Unga wa mchele 500g
Samli 250g
Sukari 250g
Hiliki iliyosagwa 1/2
kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 1/2
kijiko cha chai
Baking powder 1
kijiko cha chai
Mayai 4
Maji ya baridi 1/2
kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya
unga wa mchele, baking powder, hiliki
na sukari.
2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi
kama maji mimina kwenye ule
mchanganyiko wa unga wa mchele,
kisha uchanganye pamoja na arki.
3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea
kuchanganya mpaka unga umeanza
kuchanganyika vizuri.
4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu
kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
5. Kata kwa design unayotaka viwe
vinene visiwe kama cookies za kawaida
kama ilivyo kwenye picha na ukipenda
utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani
katikati ya kileja kama inavyoonesha
hapo juu.
6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na
350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe
vyekundu toa na tayari kwa kuliwa.
Chapisha Maoni