Asidi (Acidness)
Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa
yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali;
humaliza asidi.
Uvimbe Wa Tumbo
Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha
kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice)...
hivyo atavichanganya na juisi ya pea
iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu
anywe; ataona nafuu kubwa.
Maradhi Ya Macho
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za
panda kandokando ya macho na kope,
atafanya hivyo kabla ya kulala pamoja na
kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-
Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto au
katika juisi ya karoti.
Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha
kijiko kimoja pamoja na kijiko cha
kitunguusaumu kilichosagwa, atachangana
katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa
chumvi kidogo; atakunywa kila siku kabla ya
kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.
Kichocho (Bilharziasis)
Atakula Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja
asubuhi na jioni, yawezekana kuila Habbat-
Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja
na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia.
Ataendelea na dawa hio kwa muda wa miezi
mitatu mfululizo. Baadae atapata nguvu na
nishati.
Kutoa Wadudu Tumboni
Atakula sandwichi moto ya vitu hivi: kijiko
kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu
za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti,
pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga
(calabash), asubuhi atakunywa kinywaji cha
shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.
Utasa
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa
uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa,
atakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali
imekorogwa katika nusu kikombe cha asali,
baadae atafuatisha kunywa kikombe kikubwa
cha maziwa ya ngamia; basi inshaAllaah
itakuwa kheri.
Tezikibofu (Prostate gland)
Atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya
mgongo na atajipaka chini ya korodani
(mapumbu) na kusugua kwa mzunguko
pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko
kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane
katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji
yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote
apendao.
Pumu (Asthma)
Atanusa moshi wa mafuta a Habbat-Sawdaa
asubuhi na jioni. Pia atakula unga wake
asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku
na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni
kabla ya kulala kila siku.
Kidonda
Atayachanganya matone kumi ya mafuta ya
Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na
kijiko kimoja cha maganda ya komamanga
yaliyokaushwa na kusagwa. Atakula kila siku
kabla ya kula chakula; baadae atakunywa gilasi
ya maziwa yasiyotiwa chochote.
Saratani (Cancer)
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu
kila siku na kula kijiko cha unga wake kila
amalizapo kula katika kikombe cha juisi ya
karoti. Ataendelea hivyo kwa muda wa miezi
mitatu.
Nguvu Za Kiume

kijiko kimoja achanganye (apige) ndani ya
mayai saba ya kienyeji; atafanya hivyo siku
baada siku kwa muda wa mwezi mmoja. Basi
hata kama ana miaka 120 atapata nguvu za
barobaro!
Udhaifu kwa Ujumla
Atachukua unga wa habat sosa kiasi cha
kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari
ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote
atavichanganya katika chombo chenye asali
iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila
siku na wakati wowote apendao lakini kwa
mkate wa ngano asili.
Kuleta Hamu Ya Kula
Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa
kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno
yako, na unywe maji ya kawaida
yaliochanganywa na siki kidogo.
Kutibu Ulegevu Na Uvivu
Atakunywa- kabla ya kula – juisi ya
machungwa iliochanganywa matone kumi ya
mafuta ya Habbat-Sawdaa. Ataendelea hivyo
kwa muda wa siku kumi. Baada ya hapo
ataona nishati na uchangamfu.
Nishati akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi
Atachemsha nanaa (mint leaf), aichanganye na
asali na aingize matone saba ya mafuta ya
Habbat-Sawdaa; anywe kinywaji hiki kikiwa na
vuguvugu wakati wowote apendao. Basi
ataionea namna fahamu itakavofanya kazi.

+ coment + 5 coment
ahsante
Shukran kwa darasa zuri
Asante Sana hata ss ambao tunaanza tunajifunzia kwako
Hiyo mayai saba na unga wa habasoda .
Swali unakula hivyo hivyo mayai mabichi au unakaanga?
Kazi nzuri
Chapisha Maoni