Tumezowe kuona mama mjamzito akila sana udongo japo pia wapo ambao hua wanakula licha ya kuwa si wajawazito. Yawezekana hawa woote wanakula kutokana na hamu ambayo husikia pasipo kujua kuwa madhara yake ni makubwa kushinda hiyo hamu ambayo uwezo wa kuijuia upo chini ya mtumiaji. Nimemeona nifanye upekuzi ili nawe mwenzangu utumiae hii kitu uone faida na hasara za kutumia udongo lakini kwa bahati mbaya kwako mtumiaji faida sijapata zaidi ya hasara ambazo ni---
1.kusababisha mikwaruzo, michubuko na kupata majeraha ya ndani kwenye utumbo.
2.Ugonjwa wenye homa na maumivu makali unaojulikana kama appendicitis ambao tiba yake ni upasuaji.
3. Na pia udongo una uchafu wa kila aina vikiwemo vijidudu vya bakteria na mayai ya minyoo, hivyo kuutumia kama chakula ni hatari kwa afya ya wewe utumiaye…..
zipo hasara nyiiiiiingi ila kwasababu mi nipo kukupatia kiduuuchu,nadhani kwa leo hicho kitakutosha. Ahsante
Udongo ule una kuwa un-sterilized na hivyo uwezekano wa kupata maambuziko ni mkubwa sana.
Baadhi ni minyoo, kuna bacteria (na hatari zaidi ni TB) n.k.
Hatari kubwa zaidi inayoweza kukupeleka pabaya ASAP ni kodole tumbo. Hiki hakitibiwi kwa dawa ila operesheni pale kinapokuwa katika kiwango cha juu. Kama upo KM nyingi na hospital kinaweza kupasuka na hapo RIP inakuwa karibu nawe.
Hata kama kimeondolewa bado madhara ya infections zitokanazo na ulaji ni kubwa !
Chapisha Maoni