JITIBU TATIZO LA VIPELE KWENYE USO (CHUNUSI) KWA NJIA ZA ASILI

0 coment



Komamanga: Maganda Ya
Mkomamanga yaliyosagwa,
yakichanganywa na habbat sodah ya
unga, hutengeneza dawa nzuri ya asili
ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni
( chunusi )

Kuna idadi kubwa ya watu wanao
kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni
( Chunusi ). Kuwa na chunusi ni jambo
lenye karaha sana, kwani linakufanya
upoteze mvuto wako wa asili na hivyo
kukukosesha raha.

Zipo njia mbalimbali za asili zinazo weza
kutumika kutibu tatizo la chunusi na
vipele vya usoni.

Ifuatayo ni miongoni mwa njia bora
kabisa na ya uhakika itakayo kusaidia
kuondokana na tatizo la Chunusi au
vipele kwenye uso.

Habbat Soda : Hii ni Habbat Sodah Ya
Mbegumbegu. Habbat Sodah
iliyosagwa ndio inayo hitajika katika
kutengeneza dawa ya asili ya
kuondoa tatizo la vipele vya usoni
ama chunusi.

MAHITAJI :
i. Habbat Sawdah ya Unga iliyo sagwa.
ii.Nusu kikombe ya maganda ya
komamanga yaliyo sagwa.
iii.Nusu kikombe ya siki ya tofaha(apple )
MATAYARISHO NA MATUMIZI
Changanya na pasha moto kwa dakika
mbili kikombe kimoja cha Habbat-
Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu)
kikombe cha maganda ya komamanga
yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha
siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha
(apple).

Paka katika sehemu inayotakiwa kabla
ya kwenda kulala kila siku usiku mpaka
vipele (chunusi) vitakapoondoka.
Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka
wiki tatu na ni lazima uwekwe katika
hali ya ubaridi.
Kisiwa Cha Maarifa's photo.
HABAT SAWD

Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved