KUNGUMANGA |
katika tunda la komamanga kuna kemikali
zinazozuia kansa ya matiti isitambae mwilini.
Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarada
la Utafiti la kuzuia Kansa umeonyesha
kwamba, kemikali ziitwazo ellegitannins
zinazopatikana kwa wingi kwenye
komamanga, zinaweza kuzuia kimeng’enyo
(enzyme) aina ya aromatase, suala ambalo
huzuia kukua kwa Homoni ya estrogen
inayopatikana katika kansa ya matiti.
Shiuan Chen Kiongozi wa uchunguzi huo
amesema kwamba, kemikali hizo hupunguza
uzalishwaji wa estrogen, na kusaidia kuzuia
seli za kansa ya matiti zisizaliane mwilini,
pamoja na tezi la ugonjwa huo lisikue.
Aromatase, ni kimeng’enyo ambacho
hugeuza Homoni ya androgen kuwa
estrogen, na kushambulia kimeng’enyo
hicho ndio lengo kuu la dawa za kupambana
na kansa za matiti zinazosababishwa na
homoni ya etrogen.
Huko nyuma pia uchunguzi ulionyesha
kwamba tunda la komamanga lina faida
kubwa kiafya hasa kwa kuwa na anti
Oxidant nyingi na vitamin mbalimbali, ambalo
huzifanya tunda hilo liweze kusaidia katika
kupambana na magonjwa ya saratani,
matatizo ya moyo na hata ugonjwa wa
kusahau uzeeni au Alzheimer.
Anti Oxidant huzuiaradikali huru ambazo ni
hatari sana kwa miili yetu. Uwezo huo
hupelekea mwili kukabiliana na magonjwa
mbalimbali hata ugonjwa wa homa ya mafua
ya nguruwe. Kama huwezi kupata tunda la
komamanga sokoni, basi unaweza kutumia
juisi ya Komamanga na daima tutunze afya
zetu!
FAIDA YA JUISI YA KOMAMANGA
1. Huweza kuzuia maendeleo ya saratani
ya mapafu.
2. Hupambana na saratani ya matiti
3. Hupunguza ukuaji wa saratani ya
kibofu
4. Inaweza kuzuia na kupunguza kasi ya
ugonjwa wa Alzheimer
5. Inapunguza kolesterol
6. Hushusha shinikizo la damu
7. Hulinda meno
Inasemekana ukinywa juisi ya komamanga
(pomegranate) nusu lita kila siku kwa muda
wa mwezi mmoja, inasaidia kupunguza
mafuta tumboni kwa wale wenye vitambi.
Jitahidi kuwa na matumizi ya haya matunda
unufaike na uboreshe afya yako.
Chapisha Maoni