HISTORIA FUPI YA MTUME (S.A.W)

0 coment

HISTORIA FUPI YA MTUME (S.A.W)
JINA LAKE NA NASABU YAKE.
Jina lake ni Mohammad bin Abdallah bin Abdul mutwalib bin hashim bin Abdul manaf bin Quswai bin kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia kwa mtume Ibrahiim (A.S)
MAMA YAKE.
Mama yake ni Amina binti Wahabi bin Abdul manafi bin zuhra bin kilaab.
KUNIA YAKE NI:
Abul qaasim, pia Abuu Ibrahiim.
JINA LAKE MASHUHURI.
1- Mustafa, na anayo majina mengine mengi yaliyo pokelewa ndani ya Qur’ ani tukufu kama:
2- Khaatamun nabiyyiin. 3- Al ummiyyi. 4- Al muzammil. 5- Al mudathir. 6- Al mubiin. 7-Al kariim.
8- An nuur. 9- An niima. 10- Ar rahmaan. 11- Ash shaahid. 12- Al mubashir.13- An nadhiir. 14- Abdur rauuf. 15- Ar rahiim. 16- Ad daai na mengine mengi.
TAREHE YA KUZALIWA KAKE.
Alizaliwa tarehe 17 mwezi wa Rabiiul awwal, mwaka wa tembo sawa na mwaka 571 H.D.kutokana na kauli iliyo mashuhuri kwa mashie, na kauli nyingine inasema ya kuwa alizaliwa tarehe 12 mwezi wa Rabiul awwal mwaka huo huo.
SEHEMU ALIPO ZALIWA.
Alizaliwa katika mji wa makkatul mukarramah ulioko katika nchi ya Saudi Arabia.
KUPEWA KWAKE UTUME.
Ali pewa rasmi utume tarehe 27 mwezi wa rajab katika mji wa makka baada ya kutimiza miaka 40 ya umri wake mtukufu.
MAFUNDISHO YAKE.
Mtume (s.a.w) alikuja na wito wa usawa kwa viumbe wote, na alikuwa akilingania udugu, na msamaha kwa kila mwenye kuingia kwenye Dini ya ki islaam, kisha aliweka sheria iliyo nyepesi, na kanuni za uadilifu alizo zipokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu alie takasika, kisha waislaam wakazipokea kutoka kwa Mtume (s.a w).
MIUJIZA YAKE.
Muujiza wake pekee wa milele na milele ni Qur’ ani tukufu; ama miujiza yake iliyo dhihiri mwanzoni mwa uislaam ni mingi sana kwani hai hesabiki.
WITO WAKE.
Mtume (s.a.w) ali walingania watu kwenye upweke wa Mwenyezi Mungu katika mji wa makka na kwa njia ya siri kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kipindi cha siri ali waita watu kwa njia ya wazi kwa muda wa miaka kumi.
KUHAMA KWAKE.
Alihama kutoka katika mji wa makka kwenda madina mwanzoni mwa mwezi wa rabiul awwal baad ya kupita miaka 13 tangu kupewa utume, na kuhama huko kulitokana na maudhi mengi ya makuraishi, mushrikina na mkafiri kumuelekea yeye na maswahaba wake.
VITA VYAKE.
Mwenyezi Mungu alie takasika alimpa idhini ya kuwapiga vita mushrikina na makafiri na wanafiki, na baada ya idhini hiyo aliweza kuingia kwenye mapambano na watu hao kwenye vita vingi sana, na kati ya hivyo vilivyo kuwa mashuhuri ni Badri, Uhudi, Khandaq (Al ahzaab) Khaibar, na Hunain.
WAKEZE MTUME (S.A W).
Mtume alikuwa na wanawake kadhaa: Wakwanza ni Khadija binti Khuwailid (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake),na huyu ndie mwanamke wa kwanza wa Mtume (s.a.w), ama wengine ni : 2-Sauda binti zum’a, 3- Aisha binti abi baker, 4- Ghuzya binti dudaan (ummu shariik) 5- Hafswa binti omar, 6- Ramla binti abii sufyan (ummu habiibah), 7- Ummu salmah binti umayyah, 8- Zainab binti Juhsha, 9- Zainab binti Khaziimah, 10- Maimuna bintil Harithi, 11- Juwairia bintil Haarithi, 12- Swafia binti Hayyi bin Akhtwab.
WATOTO WAKE MTUME (S.AW).
Watoto wake ni kama wafuatao: 1- Abdallah. 2- Qaasim. 3- Ibrahiim (a.s) 4- Fatimatuz zahraa (a.s).na kuna kauli zingine zisemazo kuwa Zainab, Ruqayya, na ummu kulthum ni wanawe pia.
BABA ZAKE WADOGO.
Mtume (s.a.w) ana baba wadogo tisa (9), nao ni watoto wa abdul mutwalib kama wafuatao: 1- Al haarith. 2- Zubair. 3- Abu twalib. 4- Hamza. 5- Al ghidaaq, 6- Dharaar Al muqawwim, 7- Abu lahab. 8- Al abbas.
SHANGAZI ZAKE MTUME (S.AW).
Mtume (s.a.w) alikuwa na shangazi sita kutokana na akina mama tofauti nao ni kama wafuatao: 1- Umaimah. 2- Ummu hakiimah. 3- Burrah. 4- Aatikah. 5- Swafiyyah. 6- Arwy.
MAWASII WAKE MTUME (S.A.W).
Mawasii wake ni kumi na mbli,nao ni kama wafuatao: 1- Amirul muuminnina Ally bin abii twalib (a.s). 2- Hassan bin Ally (a.s) 3- Hussein bin Ally (a.s) 4- Ally bin Hussein (a.s). 5- Mohammad bin Ally ( a.s) 6- Jaafar bin Mohammad (a.s) 7- Mussa bin Jaafar (a.s) 8- Ally bin Mussa (a.s) 9- Mohammad bin Ally (a.s) 10- Ally bin Mohammad (a.s) 11- Hassan bin Ally (a.s) 12- Al hujjat binil Hassan (Mohammad mahdii ) (a.s).
MLINZI WAKE.
Mlinzi wake alikuwa ni Anas.
WAIMBAJI MASHAIRI WA MTUME (S.A.W).
1 – Hassan bin Thabiti. 2- Abdallah bin Rawaha. 3- Kaab bin Maalik.
WAADHINI WA MTUME (S.A.W).
1- Bilal Al –habashi 2- Ibnu ummu makhtuum. 3- Saad Al-qurt.
NEMBO YA PETE YA MTUME (S.A.W).
Nembo ya pete yake ilikuwa ni (( Mohmmad rasuulu llah)).
UMRI WAKE (S.A.W).
Ali ishi kwa muda wa miaka 63.
MUDA WA UTUME WAKE (S.A.W).
Utume wake ulidumu kwa muda wa miaka 23.
TAREHE YA KUFARIKI KWAKE (S.A.W).
Alifariki dunia tarehe 28 mwezi wa safar mwaka wa 11 hijiria.
SEHEMU ALIYO FIA (S.A.W).
Mtume alifia katika mji wa madinatul munawwarah.
SEHEMU ALIYO ZIKIWA (S.A.W).
Alizikiwa katika mji wa madina ndani ya nyumba yake tukufu.
Kwa ufafanuzi zaidi rejea katika kitabu Buharul an’waar juzuu ya 15-16,kwa wale wenye kufahamu lugha ya kiarabu.



“On the Day of the Judgement there will be nothing weightier in the balance of a momin than the goodness of

character. Allah dislikes an obscene and a rude talker and the bearer of a good moral character reaches to the

level of the observer of the prayer and fasting, on account of his character.”

MIUJIZA YA SAYANSI KATIKA QURANI


________________________________________

Ingawaje Mwenyezi Mungu hakututeremshia Qurani kuwa ni kitabu cha kutufunza elimu ya sayansi, lakini ndani ya kitabu hiki kisichomalizika maajabu yake, imo miujiza mingi ya kisayansi na maelezo ambayo isingewezekana kabisa kwa mtu asiyejuwa kusoma wala kuandika aliyeishi miaka elfu moja mia nne na ishirini iliyopita kuweza kuyajua. Haya yakituthibitishia kuwa hii (Qurani) ni Haki (Kweli) inayotoka kwa Al Haqi Muumba wa mbingu na ardhi Subhaanahu wa Taala.
Mwenyezi Mungu anasema;
“Sema: Ameyateremsha haya ajuaye siri za katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu”.
AL FURQAN – 6
Katika Suratul Baqarah, Mwenyezi Mungu aliwataka wale wasiokubali Qurani kuwa ni maneno Yake walete Sura moja mfano wa Sura za Qurani na wakashindwa kufanya hivyo. Ikiwa wao wameshindwa, jee aliwezaje Mtume Muhammad(SAW) aliyekuwa hajui kusoma wala kuandika? Kwa hivyo hapana shaka yoyote kuwa haya ni maneno ya Mwenyezi Mungu”.
Mwenyezi Mungu anasema;
“Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, (ingekuwa hivyo), wangefanya shaka wale wanaotaka kubadilisha haki.
Bali hizi ni Aya waziwazi (zinazokubaliwa) katika vifua vya wale waliopewa ilimu na hawazikatai Aya Zetu isipokuwa madhalimu (wa nafsi zao)”.
Al Ankabuut – 48 –49.
Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala ametujulisha katika hiki ‘Al Qur-an’, juu ya siri mbali mbali zilizomo ndani ya nafsi zetu, pamoja na zile zilizopo katika anga za juu, baharini na siri zilizopo katika sehemu za mbali. Na mara nyingi Mola wetu anatudokezea baadhi ya siri hizo, si kwa ajili ya kutusomesha elimu ya sayansi, kama nilivyoandika hapo mwanzo, bali hufanya hivyo ili kutuhakikishia kuwa Yeye ni Haki na kwamba kitabu hiki ‘Al Qur- an’ ni haki itokayo kwake ubhanahu wa Taala, na kwamba Siku ya Kiama ipo, na kwamba Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwafufua walio makaburini.
Na hii ni kwa sababu Imani ya kuwepo kwa Siku ya Kiama ni muhimu sana katika kutengenea kwa hali zetu.
Mwenyezi Mungu anasema;
“Tutawaonesha Ishara zetu katika sehemu za (nchi za) mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?”
Fusilat (Haamiym Sajdah) 53
MAJADILIANO NA PROFESA MARSHAL JOHNSON
Sheikh Abdul Majeed Al Zindani, ambaye ni bingwa katika uwanja huu wa Miujiza ya Sayansi katika Qurani anasema;
“Nilikuwa nikijadiliana na Profesa mmoja anayeitwa Marshal Johnson wa chuo kikuu cha Jafferson – Philadelphia, aliyehudhuria mojawapo ya mikutano inayozungumzia maudhui haya ya Miujiza ya Sayansi katika Qurani. Akaniuliza;
“Nini maana ya Miujiza ya Sayansi katika Qurani?”
Nikamjibu;
“Miujiza ya Sayansi katika Qurani, ni yale mambo yanayohusiana na Sayansi yaliyotajwa katika Qurani tokea miaka elfu moja mia nne na ishirini iliyopita na kugunduliwa na wataalamu wa mambo hayo katika zama zetu hizi, baada ya kupatikana kwa vyombo vya kisasa kabisa vya uchunguzi”.
Akaniuliza;
“Unaweza kunipa mfano?”
Nikamjibu;
“Naam nitakupa mfano. Nyinyi wataalamu wa mambo ya uzazi, mpaka mwanzo wa karne ya kumi na nane, mlikuwa mkidhania kuwa mtoto anakuwa keshaumbika kwa ukamilifu tumboni mwa mamake tokea pale anapoingia kwa njia ya manii (maji ya uzazi). Mikono, miguu pamoja na kichwa na viungo vyake vyote vinakuwa kamili, isipokuwa umbo lake linakuwa doogo sana, kisha anakuwa kidogo kidogo mpaka anapofikia katika hali ile anayozaliwa.”
Akasema;
“Kweli tulikuwa tukidhania hivyo.”
Nikamwambia;
“Katika mwanzo wa karne ya kumi na tisa, pale mlipoligundua yai (ovum), mkasema ;
‘La – sivyo tulikosea, bali mtoto anaumbika akiwa kamili lakini akiwa ndani ya yai”
Sheikh Al Zindani akaonesha picha, kutoka katika vitabu vya elimu ya mambo ya uzazi vikiwa ni ushahidi juu ya yale wataalamu waliyokuwa wakidhania mpaka kabla ya miaka mia moja iliyopita.

“Kisha baadaye kidogo mkasema; ‘Sasa tumegunduwa kuwa mtoto anakuwa ndani ya yai la uzazi umbo baada ya umbo, namna baada ya namna (stages)’.
“Na sisi”, akaendela kusema Sh. Al Zindani, “Tunaamini hivyo – Katika kitabu chake alichomteremshia Mtume wake Muhammad(SAW) miaka elfu moja mia nne iliyopita, Mwenyezi Mungu anasema;
“Mumekuwaje hamuweki hishima ya Mwenyezi Mungu. Na hali Yeye amekuumbeni namna baada ya namna?”
Nuh – 13 – 14

Na akasema;
“Hukuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo - katika viza vitatu. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu. Ufalme ni wake; hakuna aabudiwaye kwa haki ila Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?”
Az Zumar - 6
Si hivyo tu, bali Mwenyezi Mungu ametuelezea na kutupa majina ya namna mbali mbali ya utaratibu huo (stages), jinsi mtoto (Embryo) anavyokuwa ndani ya tumbo la mamake hali baada ya hali.
Mwenyezi Mungu anasema;
“Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.
Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.
Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la
nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.
Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa. Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa”.
AL MUUMINUN 12 – 16
Na akasema;
“ Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa,(mnaona haimkiniki kufufuliwa), basi (tazameni namna tulivyokuumbeni), kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo (Mzee wenu Nabii Adam), kisha (tukawa tunakuumbeni nyinyi) kutokana na manii (mbegu ya uhai), kisha (yanageuka) kuwa kipande cha damu iliogandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni (kudra zetu). Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha (tunakuleeni) mfikie kutimia akili (na nguvu za kiwiliwili pia). Na katika nyinyi wapo wanao kufa (kabla ya kufikia hali hiyo), na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri.
HAYO ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki, na kwamba hakika Yeye
ndiye mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Na kwamba hakika Saa itakuja hapana shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi
Mungu atawafufua walio makaburini”.
AL HAJJ- 5 – 7
Sh. Al Zindani anasema;
“Jambo linalosisimua ni yale majina yaliyotajwa katika Qurani yakielezea hali zile za mtoto anapoumbika ndani ya tumbo la mamake (stages) baada ya tone la manii kutulia katika makao yaliyohifadhika. Ukizifuatilia aya zote zinazoelezea maudhui haya utaziona kuwa Qurani imeyataja majina ya uhakika wa hali yake ilivyo. Kwa mfano;
ALAQAH – Na maana yake ni; Kipande cha damu iliogandana.

Katika kitabu chake Profesa Keith Moore wa Toronto – Canada, ameionesha picha ya mtoto anapokuwa katika hali hii kuwa ni sawa na kipande kilaini kilichoganda na kinachoning’inia.
MUDH GHAH – Na maana yake ni kipande cha nyama (kilichotafunwa) – (mfano wa ubani).
Katika vitabu vyote vya elimu ya uzazi wanaionesha picha ya mtoto (Embryo) katika hali hiyo akiwa mfano wa ubani uliotafunwa. Ingawaje ukubwa wake ni sawa na chembe ya mchele, lakini unapoitizama katika picha iliyokuzwa, utaona kuwa kati kati ya chembe hiyo pana alama mfano wa kitu kilichotafunwa kwa meno.”
Sheikh Al Zindani akaendelea kuzielezea hali hizo moja baada ya nyengine huku akizisherehesha.
Profesa Marshal baada ya kuyasikia yote hayo akasema;
“Kuna uwezekano wa namna tatu uliomfanya Muhammad aweze kusema maneno hayo”
Nikamuuliza;
“Uwezekano gani huo?”
Akajibu;
“Kwanza kabisa inawezekana kuwa uhakika huu umetokea kwa Sadfa tu.”
Nikamwambia;
“Siyo Sadfa Profesa”
Anasema Sh. Al Zindani;
“Nikamsomea aya zipatazo ishirini na tano zinazoelezea ‘stages’ kama zile, kwa mpangilio ule ule kisha nikamwambia
“Haiwezekani aya zote hizo zipangilike kwa Sadfa”.
Akasema
“Uwezekano wa pili ni kuwa labda Muhammad huyu alikuwa na microscope yenye nguvu sana iliyomwezesha kuzijua siri hizo”.
Nikamwambia;
“Profesa, nimeiona microscope ya mwanzo iliyotengenezwa kya miaka michnyuma na haikuwa na uwezo mkubwa wa namna hiyo. Isitoshe, inajulikana wazi kuwa katika zama zile hakukuwa na viwanda vya kuweza kukusanya na kuunda hata darubini ya kawaida.”
Akasema;
“Maneno yako ni kweli, kwa hivyo hapana kilichobaki isipokuwa uwezekano mmoja tu, nao ni kuwa Muhammad alikuwa ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyekuwa akipata habari zote hizo kutoka kwa Yule aliyeumba kila kitu”.
WALIOPEWA ILIMU
Mwenyezi Mungu anasema;

“Na wale waliopewa ilimu wanafahamu ya kuwa yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako ndiyo haki, nayo huongoa katika njia ya Mwenyezi Mungu , Asifiwaye”

Surat Saba - 6
Na anasema;
“Lakini Mwenyezi Mungu anayashuhudia aliyo kuteremshia wewe. Ameyateremsha
kwa kujua kwake (kwa elimu Yake) - na Malaika pia wanashuhudia. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.”
ANNISAA- 166
Na akasema;
“Sema: Ameyateremsha haya ajuaye siri za katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu”.

AL FURQAN – 6
Na akasema;
“Na haya ni makumbusho yaliyo barikiwa, tuliyo yateremsha. Basi je! Mnayakataa?”
AL ANBIYAA – 50
PROFESA KEITH MOORE
Ama Profesa Keith Moore, wa Toronto – Canada, ambaye vitabu vyake kuhusu ilimu ya uzazi (embryology) vimefasiriwa kwa lugha mbali mbali na kutumiwa katika vyuo vikuu mbali mbali duniani, naye pia baada ya kuelezewa na Sh. Al Zindani juu ya hali hizo na nyinginezo, akasema;



“Nitabadilisha majina ya stages hizo katika vitabu vyangu vyote na kuyapa majina yaliyotumiwa katika Qurani, kwa sababu sisi tunaziita hali zile kuwa ni ‘stage no.1.. nk. Majina yasiyobeba maana yoyote ile, wakati katika Qurani hali hizo zimepewa majina yake ya uhakika.”

Jinsi Benki Za Kiislamu Zinavyotoa Huduma Zake


KUMEKUWA na ongezeko la benki za Kiislamu huku na kule duniani hususani katika ulimwengu wa Waislamu. Mtaalamu wa masuala ya fedha katika mfumo wa fedha wa Kiislamu bw. Mohaimin Chowdhury anaifafanua benki ya Kiislamu kunzia A mpaka Z.

Mara kwa mara Waislamu husema kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, na si dini ya imani tu ya kiroho. Kwa hali hiyo, vipengele vyote vya maisha ya mwanadamu lazima viendane ni misingi ya Uislamu.

Hii ina maana kuwa, mbali ya kufuata faradhi zilizoagizwa kwa mnasaba wa Ibada kama vile kusali Swala tano,kutowa Zaka, kufunga Mwezi wa Ramadhani na kufanya Hija, Muislamu pia hana budi kufuata misingi ambayo Uislamu umeiweka kuhusiana na mambo mengine katika maisha ya kijamii mathalani mahusiano yake na wengine kifamilia na kijamii, na masuala ya kifedha.

Kuhusiana na masuala ya fedha, financial dealings, miwili kati ya misingi muhimu mno ya Sharia ni makatazo ya kutoza au kupokea riba na kuepuka chumo la pata potea, ghara.r Kwa hali hiyo basi, ili mapato ya fedha yakubaliwe na Sharia, lazima yaepukane na riba na gharar.

Mkopo katika benki za kawaida unaombatana na sharti la marejesho ya ziada ni mfano mmojawapo wa mambo yanayokatazwa kwa udhuru wa riba na mauzo ya farasi aliyetoroka ni mfano wa tijara zilizoharamishwa kwa udhuru wa gharar.

Huduma zitolewazo na Benki ya Kiislamu hufanana na zile za mabenki ya kawaida kama vile ukopeshaji wa fedha lakini japo zote hulenga shabaha moja ya kiuchumi, bado hutofautiana kwa jinsi benki za Kiislamu zinavyoendeshwa kwa mfumo unaozingatia Shariah.

Mfumo wa sasa wa Benki za Kiislamu wasemekana ulianza na benki ya Akiba, savings bank kwa msingi wa kasma ya faida (kugawana faida), profit sharing, mfumo ambao ulianzishwa nchini Misri mwaka 1963.

Inakisiwa kuwa hadi kufikia leo, kuna zaidi ya taasisi 200 za fedha za Kiislamu duniani zenye ziada ya hisa (excess) inayofikia dola za Marekani bilioni mia mbili ($200 billion).

Taasisi nyingi kati ya hizi ziko mashariki ya kati na Kusini Kaskazini mwa Asia. Hata hivyo, benki nyingi za Magharibi kama vile Citigroup,HSBC, Standard Chartered Bank na Deutsche Bank zote zina taratibu za kibenki za Kiislamu.

Nchini Uingereza, Benki ya Kiislamu ya Llyods TBS and HSBG hutoa huduma za rejareja za benki za Kiislamu. Mbali na hivyo, baadhi ya benki za kawaida za Mashariki ya kati zinazo au zinapanga kubadili taratibu zao ili ziwe za Kiislamu

Benki za Kiislamu huchukua sura tofauti. Kuna benki za rejareja kama vile Benki ya Kiislamu ya Bratain na benki za uwekezaji kama vile Arcapita (Benki ya kwanza ya uwekezaji ya Kiislamu) ambayo ipo nchini Bahrain na benki nyingine ya aina hiyo ipo Ulaya ambako imeomba kibali cha kuendesha shughuli zake na hiyo ndiyo inayotazamia kuwa benki huru ya kwanza ya uwekezaji ya Kiislamu barani Ulaya itakayoasisiwa na kuendeshwa kwa msingi kamili ya Shariah. Huduma zitakazotolewa zitazingatia aina ya benki yenyewe.

Benki ya Rejareja yenyewe huhudumia watu mmoja-mmoja na hushughulika na biashara ndogondogo, kwa hiyo, benki hii itakuwa na huduma zinazohusina na makundi haya ya wateja.

Yaweza kutoa huduma ya akaunti za muda, current accounts, akaunti za akiba, savings accounts, Huduma za uwezeshaji wa Mipango binafsi,Home Purchase Plans na Huduma za Fedha kwa Mteja, consumer financing products.

Akaunti za muda huendeshwa kwa msingi wa qard (mkopo usio na riba) kutoka kwa mteja kwenda benki huku benki ikikubali kurejesha kiasi cha fedha ilichokopeshwa na mteja pale kinapohitajika na kurejesha haki ya mteja kutumia fedha zake papo hapo.

Akaunti za Akiba, kwa kawaida, huendeshwa kwa msingi wa mudaraba ambapo mteja huweka fedha benki ili benki itumie maarifa yake kuzalisha fedha zaidi na kurejesha kiasi hicho.

Faida inayozalishwa na fedha hizo hukasimiwa (hugawanywa) kwa kiwango kilichoafikiwa hapo kabla baina ya mteja na benki, pre-ageed ratio between the customer and the bank.

Zipo njia mbalimbali ambazo mali binafsi inaweza kuendeshwa kibiashara. Njia iliyozoeleka zaidi ni Ijara ambapo benki hununua mali na kisha kuikodisha kwa mteja. Papo hapo benki hutoa ahadi ya kuuza mali hiyo kwa bei sawa na ile ile ambayo ilinunulia mali hiyo baada ya mteja kukamilisha malipo.

Kila mwezi mteja huilipa benki kodi ya kukalia mali hiyo na pia hulipa kiasi maalum kwa ajili ya ununuzi wa mali hiyo hapo baadae kutoka benki hiyo.

Nazo huduma za fedha kwa wateja, kwa mfano kugharamia ununuzi wa gari au bidhaa, huendeshwa kwa msingi wa murabaha ambapo benki hununua kitu husika kutoka kwa muuzaji na kukiuza kwa bei inayozidi kidogo ile bei iliyonunulia kitu hicho. Mteja anayeuziwa kitu hicho na benki hulipa bei ya manunuzi kwa kipindi mahususi kilichoafikiwa na pande zote mbili.

Nayo Benki ya Uwekezaji Investment Bank, kwa upande wake, hushughulika na benki na asasi nyingine za fedha, makampuni makubwa, vyombo vya serikali, na watu wenye mitaji mikubwa, high net worth individuals.

Misingi ya Uislamu ya utoaji fedha ni ile ile lakini huduma za mabenki haya zinahusika na watu wenye viwango vikubwa vya fedha. Hasara ya huduma hizi kubwa kwa kawaida huhusisha na benki nyingine (zikiwemo benki za rejareja) kwa kushirikisha huduma ili benki nyingi zichangie katika fungu la fedha zitolewazo ambapo nazo hupata sehemu ya faida itokanayo na huduma.

Ufuataji wa Sharia katika benki za Kiislamu, kwa kawaida, hufanikishwa na benki kwa kuteua bodi ya usimamizi wa Sharia inayoundwa na wanazuoni ambao wamebobea katika sheria za biashara, hawa ndio wanaosimamia shughuli za benki.

Bodi za Sharia katika benki ndizo zinazopitia na kupitisha huduma na kutowa muongozo juu ya shughuli za benki. Bodi hizi, mara nyingi, hufanya uhakiki wa shughuli ili kuhakikisha kuwa taratibu na hukumu za Sharia zinafuatwa.

Aidha wapo washauri ambao hutoa rai juu ya ufuwataji wa Sharia katika huduma yoyote au katika mkataba wowote, wakifanya kazi kama wafanyavyo kazi washauri wa kisheria wa benki nyingine.

Washauri hawa ni muhimu zaidi kwa vyombo vidogo vidogo ambavyo haviwezi kumudu gharama za kuwa na bodi ya usimamizi wa Sharia kutokana na udogo wa vyombo hivyo.

Mbali na miundo ya msingi ya shughuli za fedha za Kiislamu kama murabaha, mudaraba na ijara, benki za Kiislamu na taasisi za fedha za Kiislamu hivi sasa zinazidi kuwa na mifumo mipya. Mathalani Sukut ambao ni mbadala wa mikataba ya kawaida.

Hii hutumiwa zaidi na makampuni makubwa na vyombo vya serikali kuzalisha fedha zaidi. Muundo uliozoeleka zaidi ambao umekuwa ukitumika katika masoko ni Sukut al ijara ambao unahusisha uzunguushaji wa fedha kwa njia ya wawekezaji (hasa benki na taasisi za fedha) kwa kununua mali ambazo hukodishwa kwa kampuni au chombo cha serikali.

Miundo mingi ya Sukut ni rahisi kuendesheka kibiashara (tradable) ikiwapatia wawekezaji aina nyingine ya huduma ya uwekezaji wa Kiislamu kwa njia ya kununua na kuuza.

Vile vile katika masoko ya fedha ya Kiislamu kunajitokeza vyombo vya fedha vinavyofanana na vyombo vya kawaida, conventional derivatives. Hivi ni vyombo vya fedha ambavyo hupata faida kutokana na faida ya mali ya msingi.

Mfano mmojawapo ni Fursa huru (option) ambayo humpa mnunuzi haki (si shinikizo) kununua mali kwa bei maalum na kwa kipindi maalum. Thamani ya mali wakati wowote uwao hutegemea bei ya mali husika sokoni.

Ingawaje wanazuoni wengi wa Sharia wanaamini kuwa fursa huru haziendani na Sharia, hivi sasa vipo vyombo ambavyo vinafaida na vinaendana kabisa na Sharia ambapo watu wengi katika uchumi wa benki, banking industry, wanalitazamia eneo hili kushamiri zaidi katika muda mfupi tu ujao.

Baadhi ya Istilahi za Kibenki za Kiislamu (Islamic Banking Terms)

-Istisna: hii ni aina ya mkataba wa mauziano ambapo upande mmoja hushughulika kutengeneza kitu fulani kwa thamani ya bei ya mauzo ya kitu hicho.

-Ijara: ni muktadha wa biashara ambapo mmiliki wa kitu humkodishia mtu mwingine kwa malipo ya kodi.

-Mudaraba: ni muktadha wa biashara ambapo upande mmoja huchangia mtaji na upande mwingine huuendesha (huuzunguusha) mtaji huo. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wastani ulioafikiwa na pande husika hapo kabla lakini hasara nayo pia humpata mchangiaji isipokuwa labda isababishwe na uzembe au upumbavu wa Muendeshaji.

-Murabaha: mauzo ya kitu au bidhaa kwa bei kubwa pamoja na kiasi cha faida (Profit mark-up) kilichoafikiwa.

-Musharaka: huu ni Mpango wa Ubia (partnership) ambapo wabia (partners) huchangia mtaji kwa ajili ya mradi na wote hugawana faida au wote hupata hasara.

-Qard: Huu ni mkopo usio na riba

-Salam: Huu ni mkataba wa mauziano ya bidhaa ambapo gharama za manunuzi hulipwa kwanza halafu bidhaa hutolewa baadae katika tarehe maalum.



Ishara Na Miujiza Ya Mwenyezi Mungu




Katika maisha ya wanaadamu wote, kutoka wakati wa ujana na utoto hadi wakati wanapofariki, ishara za Mwenyezi Mungu mmoja peke Yake wa kweli zinaonyeshwa kwao katika maeneo yote ya ardhi, hata katika nafsi zao mpaka ibainike kwao kuwa yupo Mwenyezi Mungu mmoja tu wa kweli (Allah). Mwenyezi Mungu Anasema katika Qur’ani:

“Tutawaonyesha Ishara Zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi wa kila kitu?” (41: 53).

Hapa tunatoa mfano jinsi Mwenyezi Mungu Anavyompatia ishara mtu mmoja kwa upotevu kwa kuabudu masanamu. Katika eneo la kusini mashariki mwa msitu wa Amazon huko Brazil, Amerika Kusini, kabila la asili lisiostaarabika lilijenga kibanda kipya ili kumpatia makazi sanamu-mtu, Skwatch, likiwakilisha mungu mkubwa kabisa wa uumbaji wote. Siku ya pili kijana mmoja aliingia katika kibanda hicho ili kutoa heshima zake kwa mungu. Alipokuwa katika hali ya kusujudu kwa jinsi alivyofundishwa kuwa hilo sanamu ni muumba na mlezi wake, na mwenye kuruzuku, mara aliingia mbwa mzee, hafifu na mwenye upele na aliyejawa na viroboto kwenye kibanda hicho. Kijana huyo alinyanyua uso wake kwa wakati muafaka, wakati tu wakumuona mbwa huyo akinyanyua mguu wake wa nyuma na kulikojolea sanamu hilo. Kijana alimfukuza mbwa huyo katika hekalu kwa ghadhabu kubwa mno; lakini hasira na ghadhabu ilipofifia alitambua kuwa sanamu hawezi kuwa mola wake mlezi wa ulimwengu mzima. Mwenyezi Mungu ni lazima awe kila pahala, alihitimisha. Ajabu kama inavyoonekana, mbwa kulikojolea sanamu ilikuwa ni ishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kijana huyo. Ishara hii ilikuwa na risala ya Mwenyezi Mungu kuwa anachokiabudu ni cha uwongo. Tukio hili lilimuacha huru kijana huyo na utumwa wa kufuata ada alizofundishwa za kuabudu mungu wa uwongo. Matokeo yake ni kuwa huyu kijana alichaguzishwa: ama kutafuta mungu wa kweli au kuendelea katika upotevu wa njia zake.

Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatutajia kiu aliyokuwa nayo Nabii Ibraahim (‘Alayhis Salaam) katika juhudi ya kumtafuta Mwenyezi Mungu kama mfano wa wale wenye kufuata ishara Zake jinsi wanavyoongoka (na hivyo kufuata njia nyoofu na ya sawa). Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

“Na kadhaalika Tulimwonyesha Ibraahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini. Na ulipomuingilia usiku akiona nyota, akasema: Huyu ni Mola Mlezi wangu. Ilipotua akasema: Siwapendi wanaotua. Alipouona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu waliopotea. Na alipoliona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola lezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipotua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayofanyia ushirikina. Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliyeziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina” (6: 75 – 79).

Kama ilivyotajwa hapo awali, Manabii walitumwa kwa kila taifa na kabila kuunga mkono itikadi ya kimaumbile ya mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu na mwelekeo wa silica aliozaliwa nao mwanadamu wa kumuabudu Yeye, vile vile kutilia nguvu ukweli wa kutoka kwa mungu.

Kwa ishara za kila siku zilizodhihirishwa na Mwenyezi Mungu. Japokuwa mafunzo mengi ya Manabii hawa yaligeuzwa, sehemu zinazoonyesha vifungu zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu zimebaki bila ya waa na zimewatumikia wanaadamu kuwaongoza katika kuchagua baina ya ukweli na uwongo, na haki na batili. Ushawishi wa risala zilizofunuliwa na Mwenyezi Mungu kupitia kwa zama zote zinaweza kuonekana katika “Amri Kumi” za Uyahudi katika Taurati ambazo baadaye zilichukuliwa na kuingizwa katika mafunzo ya Ukristo. Vile vile kuwepo kwa kanuni dhidi ya mauaji, wizi na uzinzi katika jamii nyingi sana kote duniani, katika zama za kale na sasa.

Matokeo kwa ishara za Mwenyezi Mungu kwa wanaadamu kupitia kwa zama zote zikichang’anywa na wahyi Wake kupitia kwa Manabii Wake, wanaadamu wote wamepatiwa fursa ya kumtambua Mwenyezi Mungu mmoja tu wa kweli.

Kwa hiyo, kila nafsi itahesabiwa kwa itikadi yake kwa Mwenyezi Mungu na kukubali kwake kwa Dini ya kweli ya Mwenyezi Mungu, Uislamu, ambayo ina maana ya kunyenyekea na kutii amri za Allah (Subhaanahu wa Ta'ala).








HISTORIA FUPI YA MTUME (S.A.W)
JINA LAKE NA NASABU YAKE.
Jina lake ni Mohammad bin Abdallah bin Abdul mutwalib bin hashim bin Abdul manaf bin Quswai bin kilaab. Na ukoo wake mtukufu unamalizikia kwa mtume Ibrahiim (A.S)
MAMA YAKE.
Mama yake ni Amina binti Wahabi bin Abdul manafi bin zuhra bin kilaab.
KUNIA YAKE NI:
Abul qaasim, pia Abuu Ibrahiim.
JINA LAKE MASHUHURI.
1- Mustafa, na anayo majina mengine mengi yaliyo pokelewa ndani ya Qur’ ani tukufu kama:
2- Khaatamun nabiyyiin. 3- Al ummiyyi. 4- Al muzammil. 5- Al mudathir. 6- Al mubiin. 7-Al kariim.
8- An nuur. 9- An niima. 10- Ar rahmaan. 11- Ash shaahid. 12- Al mubashir.13- An nadhiir. 14- Abdur rauuf. 15- Ar rahiim. 16- Ad daai na mengine mengi.
TAREHE YA KUZALIWA KAKE.
Alizaliwa tarehe 17 mwezi wa Rabiiul awwal, mwaka wa tembo sawa na mwaka 571 H.D.kutokana na kauli iliyo mashuhuri kwa mashie, na kauli nyingine inasema ya kuwa alizaliwa tarehe 12 mwezi wa Rabiul awwal mwaka huo huo.
SEHEMU ALIPO ZALIWA.
Alizaliwa katika mji wa makkatul mukarramah ulioko katika nchi ya Saudi Arabia.
KUPEWA KWAKE UTUME.
Ali pewa rasmi utume tarehe 27 mwezi wa rajab katika mji wa makka baada ya kutimiza miaka 40 ya umri wake mtukufu.
MAFUNDISHO YAKE.
Mtume (s.a.w) alikuja na wito wa usawa kwa viumbe wote, na alikuwa akilingania udugu, na msamaha kwa kila mwenye kuingia kwenye Dini ya ki islaam, kisha aliweka sheria iliyo nyepesi, na kanuni za uadilifu alizo zipokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu alie takasika, kisha waislaam wakazipokea kutoka kwa Mtume (s.a w).
MIUJIZA YAKE.
Muujiza wake pekee wa milele na milele ni Qur’ ani tukufu; ama miujiza yake iliyo dhihiri mwanzoni mwa uislaam ni mingi sana kwani hai hesabiki.
WITO WAKE.
Mtume (s.a.w) ali walingania watu kwenye upweke wa Mwenyezi Mungu katika mji wa makka na kwa njia ya siri kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya kipindi cha siri ali waita watu kwa njia ya wazi kwa muda wa miaka kumi.
KUHAMA KWAKE.
Alihama kutoka katika mji wa makka kwenda madina mwanzoni mwa mwezi wa rabiul awwal baad ya kupita miaka 13 tangu kupewa utume, na kuhama huko kulitokana na maudhi mengi ya makuraishi, mushrikina na mkafiri kumuelekea yeye na maswahaba wake.
VITA VYAKE.
Mwenyezi Mungu alie takasika alimpa idhini ya kuwapiga vita mushrikina na makafiri na wanafiki, na baada ya idhini hiyo aliweza kuingia kwenye mapambano na watu hao kwenye vita vingi sana, na kati ya hivyo vilivyo kuwa mashuhuri ni Badri, Uhudi, Khandaq (Al ahzaab) Khaibar, na Hunain.
WAKEZE MTUME (S.A W).
Mtume alikuwa na wanawake kadhaa: Wakwanza ni Khadija binti Khuwailid (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake),na huyu ndie mwanamke wa kwanza wa Mtume (s.a.w), ama wengine ni : 2-Sauda binti zum’a, 3- Aisha binti abi baker, 4- Ghuzya binti dudaan (ummu shariik) 5- Hafswa binti omar, 6- Ramla binti abii sufyan (ummu habiibah), 7- Ummu salmah binti umayyah, 8- Zainab binti Juhsha, 9- Zainab binti Khaziimah, 10- Maimuna bintil Harithi, 11- Juwairia bintil Haarithi, 12- Swafia binti Hayyi bin Akhtwab.
WATOTO WAKE MTUME (S.AW).
Watoto wake ni kama wafuatao: 1- Abdallah. 2- Qaasim. 3- Ibrahiim (a.s) 4- Fatimatuz zahraa (a.s).na kuna kauli zingine zisemazo kuwa Zainab, Ruqayya, na ummu kulthum ni wanawe pia.
BABA ZAKE WADOGO.
Mtume (s.a.w) ana baba wadogo tisa (9), nao ni watoto wa abdul mutwalib kama wafuatao: 1- Al haarith. 2- Zubair. 3- Abu twalib. 4- Hamza. 5- Al ghidaaq, 6- Dharaar Al muqawwim, 7- Abu lahab. 8- Al abbas.
SHANGAZI ZAKE MTUME (S.AW).
Mtume (s.a.w) alikuwa na shangazi sita kutokana na akina mama tofauti nao ni kama wafuatao: 1- Umaimah. 2- Ummu hakiimah. 3- Burrah. 4- Aatikah. 5- Swafiyyah. 6- Arwy.
MAWASII WAKE MTUME (S.A.W).
Mawasii wake ni kumi na mbli,nao ni kama wafuatao: 1- Amirul muuminnina Ally bin abii twalib (a.s). 2- Hassan bin Ally (a.s) 3- Hussein bin Ally (a.s) 4- Ally bin Hussein (a.s). 5- Mohammad bin Ally ( a.s) 6- Jaafar bin Mohammad (a.s) 7- Mussa bin Jaafar (a.s) 8- Ally bin Mussa (a.s) 9- Mohammad bin Ally (a.s) 10- Ally bin Mohammad (a.s) 11- Hassan bin Ally (a.s) 12- Al hujjat binil Hassan (Mohammad mahdii ) (a.s).
MLINZI WAKE.
Mlinzi wake alikuwa ni Anas.
WAIMBAJI MASHAIRI WA MTUME (S.A.W).
1 – Hassan bin Thabiti. 2- Abdallah bin Rawaha. 3- Kaab bin Maalik.
WAADHINI WA MTUME (S.A.W).
1- Bilal Al –habashi 2- Ibnu ummu makhtuum. 3- Saad Al-qurt.
NEMBO YA PETE YA MTUME (S.A.W).
Nembo ya pete yake ilikuwa ni (( Mohmmad rasuulu llah)).
UMRI WAKE (S.A.W).
Ali ishi kwa muda wa miaka 63.
MUDA WA UTUME WAKE (S.A.W).
Utume wake ulidumu kwa muda wa miaka 23.
TAREHE YA KUFARIKI KWAKE (S.A.W).
Alifariki dunia tarehe 28 mwezi wa safar mwaka wa 11 hijiria.
SEHEMU ALIYO FIA (S.A.W).
Mtume alifia katika mji wa madinatul munawwarah.
SEHEMU ALIYO ZIKIWA (S.A.W).
Alizikiwa katika mji wa madina ndani ya nyumba yake tukufu.
Kwa ufafanuzi zaidi rejea katika kitabu Buharul an’waar juzuu ya 15-16,kwa wale wenye kufahamu lugha ya kiarabu.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved