Kwanini uende massage
lounge?
Binadamu wote lazima tuchoke wakati fulani na
kupata maumivu ya viungo vya miili yetu.Basi si kila
siku tuwe tunakimbizana kwenye massage
lounge,siku moja moja unatakiwa umsugue na
kumchua mwenzio nyumba.
Oga vizuri kabla ya kuanza shughuli hii, inaweza
fanywa kitandani, kwenye mkeka au chini palipo
tandikwa vizuri. Unaanza kuusugua mwili wote
kwanza kwa kutumia unga wa liwa na unga wa
karafuu ulichanganywa na maji ya rose na mafuta
ya miski. Sugua mwili mpaka uhisi uchafu na
nongo zote zimeisha.Baada ya hapo unaoga
nakurudi kwa ajili ya kuuchua mwili.Unaweza
chukua mafuta ya mzaituni,ya nazi,ya karafuu,ya
ufuta au ya mchaichai unampaka mwili mzima na
kuanza kumchua(kummassage) taratibu bila
kutumia nguvu,tumia mda mwingi kuchua sehem
za mgongoni na kiunoni.Utaendelea kumsinga
mpaka utakaporidhika,baada ya hapo shughuli ya
kusinga itakua imeisha.
Kusugua na kuchua mwili inasaidia kuondoa
uchafu mwilini,kupunguza maumivu makali
mwilini,inakufanya upate pumziko na kuondoa
msongo wa mawazo , kutaiwezesha mishipa ya
damu kuwa katika hali nzuri na hivyo kurahisisha
msukumo wa damu katika mwili wako.Pia huleta
furaha kwa wale wawili wapendanao.
MUHIMU:
Mafuta ya karafuu na Unga Wa
karafuu Vinawasha kwahiyo kua makini visiguse
sehem za siri na machoni.
Chapisha Maoni