Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery
amepeana agizo kwa polisi kukamata gari
lolote lililo na king’ora ama taa maalumu
zinazotumika na king’ora ambazo
zimewekwa kinyume cha sheria.
Katika taarifa yake, Nkaissery amesema
hakuna yeyote anayeruhusiwa kuwa na
king’ora a,a taa hizo kwenye gari lake
ispokuwa rais na naibu wake. Akiongezea
kuwa magari mengine yanayoruhusiwa
kuwa na vifaa hivyo ya polisi, ambulesi na
yale ya wazima moto.
Nkaissery amesema kuna magari mengi ya
kibinafsi yaliopachikwa vifaa hivi ilihali hilo ni
kinyume cha sheria. Magari ya huduma za
mazishi zimekuwa na tabia ya kutumia hasa
taa hizo. Hilo ni kukiuka sheria. Baadhi ya
wanasiasa pia hutumia ving’ora ili kupata
mpenyo wakati wa msongamano wa magari.
Chapisha Maoni