MUISLAMU KUFUGA RASTA INAKUBARIKA?????
0 coment
Swali:mimi niliuliza swali je inaruhusiwa kisharia kwa mwanamke au mwanamume kuwa na rasta zake asilia JIBU:kuweka rasta ni kuwaiga wasio kuwa waislam na sikatika mila zetu katika iman Uislamu unachunga nadhafa na usafi na mienendo yote kama tulivyofundishwa na mtume S.A.W yeye ndie aliye tukataza tusijifananishe au kuwaiga wasiokuwa waislam Kuhusu kujifananisha nao mtume amesema Atakaejifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao .ABUU DAAWUUD na AHMAD isitoshe hali hii inaharibu maumbile ya asili ambayo ni uislam Hivyo kuweka rasta ni jambo lisilo la kiislam na halifai na swali la kuwauliza wafanyao hivyo wanafanya kwa malengo yapi? kwa mafunzo ya nani? Ikiwa pia kuvutiwa kwa kuwaona hao ambao sehemu ya dini yao ni kuvuta bangi basi hakika mtu huyo atakuwa hajitambui na hajui malengo yake hapa duniani na kwasababu malengo ya mwanadamu hapa ulimwenguni ni kumuabudu mungu na hakupatikani hilo ispokuwa mtu kuwa muislam na kufuata mafunzo yote bila kuacha mengine Tunamuomba mwenyezimungu awaongeze waislamu na awaruzuku mapenzi ya kuipenda dini yao na kuifuata na kuacha mila tamaduni zisizo kuwa za KIISLAM Mungu anajua zaid
Chapisha Maoni