"Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope, kwa kuwa BWANA Mungu wako yu pamoja nawe, aliyekukweza katika nchi ya Misri. Na iwe msongeapo mapiganoni, Kuhani na kusema na watu, awaambie, sikizeni, enyi Israili, hivi leo mwasongea mapiganoni juu ya adui zenu; mioyo yenu isizime, msiache wala msitetemeke, wala msiingiwe na hofu kwa ajili ya wao. Kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi".
(Kumb. 20:1-4)
Jihadi rasmi ya kwanza kabisa iliongozwa na Nabii Yoshua mwana wa Nuni, ili kuwaingiza Waisraeli katika nchi ya ahadi (Kaanani) wakitokea Misri. Mji wa kwanza kushambuliwa ulikuwa wa Yeriko. Kwanza Yoshua (a.s.) alipeleka wapelelezi wawili ambao walijificha katika nyumba ya kahaba Rahabu (Yoshua 2:1-24). Kisha waliuvamia mji na kuuweka "Wakfu" kwa kuua kile chenye uhai isipokuwa kahaba Rahabu na familia yake.
"...Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee na ng’ombe, na kondoo, na punda kwa makali ya upanga".
(Yoshua 6:21)
Na Yoshua 6:24 inasema;
…Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake…
Utaratibu wa "kufyagia" miji uliendelea hadi Yoshua mwana wa Nuni alipotawala miji yote aliyoitaka. (Yoshua 10:28; 11:16-23).
Wakuu wa nchi (wafalme) wao walikumbana na vifo vya aina yake;
"Kisha ikawa hapo walipomletea Yoshua hao wafalme watano hapo nje, Yoshua akawaita wanaume wote wa Israeli, akawaambia majemedari wa vita waliokwenda naye, haya jongeeni karibu, mweke nyayo za miguu yenu katika shingo za wafalme hawa. Nao wakajongea karibu, wakatia nyayo zao katika shingo zao. Yoshua akawaambia., msiache wala msifadhaike, iweni hodari, na mioyo ya ushujaa, kwa kuwa ndivyo BWANA atakavyowafanyia adui zenu wote, ambao mwapigana nao. Baada ya Yoshua akawapiga na kuwaua, akawatundika katika miti mitano, nao wakawa wakitundikwa katika miti hiyo hata jioni".
(Yoshua 10:24-26).
Aidha, wakati mwingine Yehova, alishiriki yeye binafsi "kuua" watu wengi zaidi kuliko "walivyouawa" kwa mikono ya watu wake.
"Kisha ikawa hapo walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli, hapo walipokuwa katika kutelemkia Beth-horoni, ndipo BWANA alipowatupia mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao hata kufikilia Azeka, nao wakafa, hao waliokufa kwa kuuawa na hayo mawe ya barafu walikuwa ni wengi kuliko waliouliwa na wana wa Israeli kwa upanga".
(Yoshua 10:11)
Na Yuda walipo tazama nyuma, angalia, vita vikawa mbele na nyuma; wakamlilia BWANA na makuhani wakapiga mapanda. Ndipo wakapiga kelele na watu wa Yuda; ikawa. Watu wa Yuda walipopiga kelele, Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda. wana wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda; naye Mungu akawaua mikononi mwao. Abiya na watu wake wakapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli mia tano elfu, watu wateule. Ndivyo walivyo tiishwa watu wa Israeli wakati ule, wakashindwa wana wa Yuda, kwa kuwa walimtegemea BWANA, Mungu wa baba zao. Abiya akamfuata yeroboamu, akamnyang'anya miji, betheli na miji yake, na Yeshana na miji yake, Efroni na miji yake. wala Yeroboamu hakupata nguvu tena siku za Abiya; kisha BWANA akampiga akafa. ila Abiya akapata nguvu akapata nguvu akaoa wake kumi na wanne, akazaa wana ishirini na wawili binti kumi na sita.
2 Nyak, 13:14-21
Jihadi ya kuikomboa nchi ilianza mwaka 1220 KK na kuendelea hadi mwaka 1010 KK ambapo Nabii Daud (a.s.) aliutwaa mji wa Yerusalem na kuwa makao makuu ya dola yake. Dola hii ilidumu kwa muda wa miaka 290 kwa dola ya Kaskazini (Samaria) na miaka 423 kwa dola ya kusini (Yuda). Dola hizi zilianguka na kutawaliwa na mapagani baada ya kumwasi Yehova, kwa kufuata sheria zisizo za Mungu. Baada ya kuteswa sana na mapagani walianzisha tena jihadi ili kujikomboa wakati wa mfalme Mgiriki Antioko Epifani (175 – 163 KK). Vita hivi vilianzishwa rasmi na Matathia mwaka 166 KK. Sababu ya kuanzishwa kwa jihad hii ilikuwa kurejesha sheria za Torati zilizofutwa na Antioko Epifani ili kuleta "Umoja na mshikamano wa kidola (Empire)".
"Mfalme Antioko akaziandikia milki zake zote, kwamba wote wawe taifa moja, kila mtu aache sheria zake za asili. Watu wote wa mataifa wakaikubali amri ya mfalme, hata wengi katika Israel (Waislamu) walifuata ibada yake, wakitoa dhabihu kwa miungu ya uongo na kutia najisi sabato. Mfalme akapeleka barua Yerusalemu na kwenye miji ya Uyahudi (dola ya Kiislamu) kwamba wazifuate desturi zilizo za kigeni kwao, waache kutoa sadaka za kutetekezwa a dhabihu na sadaka ya kinywaji hekaluni, wazinajisi sabato na sikukuu, na kulitia unajisi hekalu na waliotakasika. Tena, wajenge madhabahu na mahekalu na viwanja vitakatifu vya miungu ya uwongo, na kutoa dhabihu za nguruwe na wanyama wachafu, waache wana wao bila kutahiriwa, na kujitia nafsi zao unajisi kwa uchafu na ukafiri wa kila namna, kusudi waisahau sheria (Torati) na kuzibadili kawaida zao. Naye asiyelitii neno la mfalme atakufa".
(1 Makabayo 1:41-50)
Kuhani Matathia hakuvumilia kuendelea kuona fedheha hiyo dhidi ya waumini na akasema:
"(Mathathia) akayaona mambo ya ukufuru yaliyotendeka katika Uyahudi na Yerusalemu, akasema, ole wangu! Kwa nini nalizaliwa kuuona uharibifu wa watu wangu na maangamizo ya mji mtakatifu, hata kukaa kimya unapotiwa katika mikono ya adui zake, na patakatifu pake (Msikiti mkuu - Hekalu) katika mikono ya wageni (Antioko aliteka hekalu na kulinajisi kwa kuingiza madhabahu yake ya kutambikia maarufu "chukizo la uharibifu"). Nyumba yake imekuwa kama ya mtu asiye na heshima vyombo vyake vya fahari vimetekwa na kuchukuliwa; watoto wake wameuwawa njiani, na vijana wake kwa upanga wa adui taifa lipi lisiloyashiriki mateka yake? Ufalme upi usioziteka mali zake? Mapambo yake yote yameondolewa naye aliyekuwa muungwana amekuwa mtumwa! Naaam, vyombo vitakatifu vyetu na fahari yetu na utukufu wetu vimefanywa ukiwa; vimetiwa unajisi na watu wa mataifa. Mbona, basi, tuzidi kuishi? Matathia na wanawe wakararua nguo zao, wakajivika gunia, wakalia kwa majonzi (toba ya kweli)
(1 Makabayo 2:6-14).
"Baada ya toba hiyo ya kweli akatangaza jihadi "kisha, Matathia alipiga mbiu mjini kwa sauti kuu, akisema, kila aliye na juhudi (mujahid) kwa ajili ya sheria (Torati) na kutaka kulitetea agano, na ANIFUATE! Naye na wanawe wakakimbilia, wakaviacha vyote walivyokuwa navyo mjini"
(1 Mak. 2:27-28).
Kisha kazi ikaanza. Baadhi ya Wayahudi wapatao 1000 walienda kujificha jangwani. Askari wa mfalme waliwafuata katika siku ya sabato kwa kuogopa "kuinajisi" sabato walisita kupigana na wote wakachinjwa kama mbuzi (tazama 1Mak 2:29-38).
Lakini kuhani Matathia akaamua hivi:
"Matathia na rafiki zake walipopata habari waliambana, kama sisi sote tutafanya kama walivyofanya ndugu zetu, tusipigane na watu wa mataifa kwa ajili ya nafsi zetu na amri (sheria) zetu, watatufata upesi katika nchi. Wakafanya shauri siku ile ya kuwa; kama mtu yeyote akituletea vita siku ya sabato TUPIGANE NAYE, tusife wote kama ndugu zetu waliokufa katika vificho vyao. Wakati huo kundi la Wahasidimu (mujahidina) walijiunga nao, Waisraeli hodari wa vita waliojitoa kwa hiyari kuitetea sheria. Na wote (wasio waumini) waliyakimbia maovu walikuja kwao na kuwaongezea nguvu. Wakakusanya jeshi kubwa, wakawapiga wenye dhambi (makafiri) katika hasira yao na, (waumini) walioasi (wanafiki) katika ghadhabu yao; na (wanafiki) waliobaki waliwakimbilia mataifa (makafiri) wajisalimishe kwao. Matathia na rafiki zake wakazunguka zunguka wakizivunja madhabhu za miungu na kutahiri kwa shuruti watoto wote wasiotahiriwa katika mipaka ya Israeli; wakawafuata wana wa uovu na kazi ilifanikiwa mikononi mwao. Wakaiokoa sheria katika mikono ya mataifa na wafalme, wasikubali wenye dhambi wainue pembe zao".
(1Mak. 2:39-48)
Kuhani Matathia alipokaribia kufa aliwausia wanawe yafuatayo:
"Msiyaogope maneno ya mtu mwenye dhambi, maana fahari yake itakuwa samadi na funza. Leo atainuka na kesho hataonekana kamwe, amerudia udongo wake na mawazo yake yamepotea. Basi ninyi wanangu, muwe hodari, mfanye kwa kiume kwa ajili ya sheria (Torati), maana kwa hiyo mtatukuzwa. Tazama, Simon ndugu yenu, najua ya kuwa ya mtu wa shauri; msikilizeni siku zote; atakuwa baba kwenu. Yuda Makabayo, shujaa tangu ujana wake, atakuwa jemadari wenu na kuwapigania watu wenu. Nanyi, wapokeeni wote wanaoishika sheria, mkatoze kisasi cha maovu waliyotendewa watu wenu. Wapatilizeni mataifa na kuyaangalia (kuyafuata) maneno ya sheria. Akawabariki, akakusanyika kwa baba zake (akafa)"
(1Mak. 2:64-69)
Yuda Makabayo akakumbana na mtihani:
"Apolonio akakusanya mataifa pamoja na watu wengi kutoka Samaria, ili apigane na Israeli. Yuda akapata habari, akaenda kukutana naye, akampiga akamuua. Watu wengi wakanguka wametiwa jereha za mauti na wengine wakakimbia. Wakateka nyara, naye Yuda aliutwaa upanga wa Apolonio, akautumia siku zote. Seroni, jemadari wa jeshi la Shamu, alisikia ya kuwa Yuda amekutanisha mkutano, jeshi la watu waaminifu (wacha Mungu) na walio hodari wa vita, akasema, nitalitukuza jina langu na kujipatia heshima katika ufalme kwa kupigana na Yuda na wale walioko kwake wanaoidharau amri ya mfalme. Na pamoja naye walikwenda jeshi kubwa la watu waovu ili wamsaidie kuwatoza kisasi wana wa Israeli. Akaja karibu na mipando ya Beth-horoni, Yuda akamwendea na kikosi kidogo. Nao walipoliona lile jeshi kubwa likija juu yao walimwambia Yuda, Je! Sisi kundi dogo tutaweza kupigana na umati huu mkubwa wa nguvu? Nasi tumedhoofu kwa sababu hatujaonja kitu leo. Yuda akasema, ni jambo rahisi watu wengi wazingiwe kwa mikono ya wachache. Kwa mbingu (Mwenyezi Mungu s.w.) ni mmoja tu, kuokoa kwa wengi au kwa wachache, maana kushinda vitani hakupatikani kwa wingi wa watu, ila kwa nguvu itokayo mbinguni. Wao wanatujia kwa wingi ni jeuri na udhalimu ili kutuharibu sisi na wake zetu na watoto wetu na kututeka. Lakini sisi tunazipigania maisha na amri zetu . Yeye (Yehova s.w.) atawafadhaisha usoni petu,basi msiwaogope. Akisha kusema hayo, aliwashambulia kwa ghafula, Seroni na jeshi lake wakapondwa mbele yake. Wakawafuatia katika mitelemko ya Beth-horoni hata uwandani chini wakaanguka watu kama mia nane na waliosalia walikimbilia nchi ya Wafilisti. Basi hofu na woga uliwaangukia mataifa ya jirani kwa sababu ya Yuda na ndugu zake, jina lake likajulikana hata kwa mfalme na mataifa yote walisimulia habari za vita vyake"
(1Mak. 3:10-26).
Jihadi hii iliendelea hadi dola yote ya kiyahudi ilipokombolewa na amani kurejea. Katika kuthibitisha kuwa Mungu, yuko pamoja na mujahidina katika vita vyao, mujahidina watatu (3) walilishinda jeshi la makafiri zaidi ya elfu kumi. (Mujahid) Yonathan na jeshi lake wakapiga kambi penye ziwa la Genesareti hata asubuhi na mapema wakaondoka kwenda uwanda wa Hazori. Jeshi la mataifa lilikutana naye uwandani. Wengine wao walikuwa wakimwotea milimani, hali jeshi lenyewe lilipambana naye uso kwa uso Nao waliomwotea wakaondoka wakajitia katika vita, na wote wa upande wa Yonathani walikimbilia, asibaki hata mmoja ila Matathia bin Absolomu na Yuda bin Kalfi, wakuu wa vikosi. Yonathani akararua nguo zake akajitia mchanga kichwani (toba ya kweli) akasali. Akajitia tena vitani, akawarudisha nyuma, hata wakakimbia, watu wake walipoona hivi walimrudia wakafuatana naye wakiwakimbiza mpaka Kadeshi kwenye kambi lao, wakatua. Siku ile katika wageni walianguka (walikufa) watu kama tatu elfu. Yonathani akarudi Yerusalem".
(1Mak 11:67-74)
1samweli 15:3 inasema:
Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni mwanaume na mwanamke, mtoto naye anyonyae, ng’ombe na kondoo ngamia na punda.
Basi ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliye mjua mume kwa kulala pamoja naye, lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye mtawaweka hai kwa ajili yenu.
Hesabu 31:17
Kumb 20:16-20
But of the cities of these people, which the LORD thy God doth give thee for an inheritance, thou shalt save alive nothing that breatheth: But thou shalt utterly destroy them; namely, the Hittites, and the Amorites, the Canaanites, and the Perizzites, the Hivites, and the Jebusites; as the LORD thy God hath commanded thee: That they teach you not to do after all their abominations, which they have done unto their gods; so should ye sin against the LORD your God. When thou shalt besiege a city a long time, in making war against it to take it, thou shalt not destroy the trees thereof by forcing an axe against them: for thou mayest eat of them, and thou shalt not cut them down (for the tree of the field is man's life) to employ them in the siege: Only the trees which thou knowest that they be not trees for meat, thou shalt destroy and cut them down; and thou shalt build bulwarks against the city that maketh war with thee, until it be subdued.
Hapa hapa lazima tujiulize kwa nini kila chenye kupumuwa kiuliwe…? Ina maana hakuna huruma hata kwa wanyama sembuse watoto na vikongwe!? Haya ndo tunayo yaona leo Iraq, Afghanistan, Chechnya na kwengineko...
Vita na maandalio ya vita yalikuwa mengi sana angalia pia 2nyaka 32:2-9 uone jinsi Hezekia alivyo funga chemchemu za maji ili mfalme wa Ashura aitwae Senakeribu ashindwe vita kwa kiu na njaa.
Isa 31:4 ...ndivyo bwana wa majeshi ataposhuka ili kufanya vita juu ya mlima sayuni, na juu ya kilima chake...
Kumb, 3:22 msimwache, kwa kuwa bwana, mungu wenu, ndiye awapiganiaye.
Inajulikana kuwa Mungu wa kwenye bibilia kesha weka ahadi yake kwa kusema;
…Mungu si mtu, aseme uongo; wala si mwanadamu ajute; iwapo amelisema, hatalitenda? iwapo amenena, hatalifikiliza?
Hes, 23:19
Huyu ndie Mungu wa kwenye biblia, na hayo nilio yanukuu ni kutoka kwenye biblia. Si ajabu kuona ivi leo mataifa ya kimagharibi yakifuata mfumo huu wa kivita toka kwenye biblia. Tuna shuhudi mengi sana toka kwenye vyombo vya habari na kuona jinsi nchi amabazo zinashambuliwa zikiangamizwa kwa mabomu na maroketi, toka nchi za kimagharibi. Watoto, wanawake wajawazito, wazee na vikongwe, wanyama na mimea hakuna kinacho salimika… yaani ni mauwaji kwenda mbele…!!
Basi kama aliahidi kuangamiza miji ataiangamiza tu, atushangahi George W. Bush kututangazia kuwa ametumwa na mungu kufanya vita na mataifa ya kiislam… atushangai kuomuona Bush akimwambia James Robison (a prominent minister) kuwa... 'I've heard the call. I believe God wants me to run for President.'
Wamarekani hawakuwa nyuma kumuunga mkono rais wao kwa kusema, ...it must have been God who selected Bush, since a plurality of voters hadn't. "Why is this man in the White House? The majority of America did not vote for him. He's in the White House because God put him there for a time such as this." (William "Jerry" Boykin.)
hata magazeti yao hakubaki nyuma Time magazine gazeti la marekani likaandika,
"Privately, Bush talked of being chosen by the grace of God to lead at that moment."
World Magazine, a conservative Christian publication, quoted White House official Tim Goeglein as saying, "I think President Bush is God's man at this hour, and I say this with a great sense of humility."
Even former President George H.W. Bush speculated that perhaps he needed to be defeated so that his son could become president: "If I'd won that election in 1992, my oldest son would not be president of the United States of America," he said. "I think the Lord works in mysterious ways."
Chapisha Maoni