Inawezekana katika maisha yako hujawahi
kula mboga iliyowekwa kiungo kinachoitwa
bizari, kama umewahi, inawezekana pia
hujawahi kujua faida zake mwilini.
Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii
ya mimea unaochimbwa kama mizizi, mfano
wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina
rangi ya njano na hujulikana pia kama
‘manjano’ kutokana na rangi yake.
Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la
Asia na hasa India na China. Kutokana na
umuhimu wake kiafya, vyakula vingi
hupikwa kwa kuchanganya na kiungo hikiambacho sasa kimeenea dunia nzima,
ikiwemo Tanzania.
FAIDA ZA BIZARI KIAFYA
Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo
cha mboga cha kuongeza ladha katika
mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna
faida nyingi unazozipata unapotumia kiungo
hiki kila mara katika mapishi yako.
Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho
vyenye uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili,
mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina
uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu
(cholesterol) na kuzuia mtu kuzeeka kabla ya
wakati.
Aidha, bizari huimarisha sehemu za magoti
hivyo kukuepusha na matatizo ya miguu
kuuma. Bizari pia hun’garisha ngozi na
kuifanya kuwa yenye afya na huimarisha pia
mfumo wa usagaji chakula (Digestion).
SUALA LA UBORA NI MUHIMU
Katika ulimwengu wa maendeleo ya sayansi
na teknolijia tulionao sasa, bizari
hutengenezwa viwandani na kuhifadhiwa
kwa usafirishaji sehemu mbalimbali duniani
na kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu.
Katika hali kama hiyo, si ajabu kukuta bizari
iliyoongezewa kemikali zingine za kuhifahdia
chakula.
Bizari ya aina hiyo, tayari inakosa faida
zilizoelezwa hapo juu, hivyo ni suala muhimu
kuangalia ubora wa bizari unayoitumia na
mahali inapotoka. Katika nchi yetu, Mungu
ametujaalia ardhi yenye rutuba ambapo
kiungo kama hiki kinalimwa na kupatikana
kwa wingi na kwa uhalisia wake.
Katika suala la kujali ubora, pendelea zaidi
kununua bizari kutoka sokoni ambayo
imetengenezwa katika mazingira safi na
salama na bila kuchanganywa na kitu
kingine. Iwapo pia utanunua bizari
iliyokwisha hifadhiwa, ni vyema ukasoma
maelezo yake kuona kama haina
vikorombwezo (additives) vingine.
Ni ukweli ulio wazi kuwa ukitumia bizari
iliyobora utapa faida nyingi kiafya, hivyo
hakikisha katika upikaji wako wa kitoweo
cha nyama, kama vile kuku, samaki, ngo’mbe
unaweka bizari. Upikaji mzuri ni ule wa
kuweka kiungo hicho mwisho baada ya
mboga yako kuchemka na kuiva, kwani
haitakiwi bizari kuchemka sana.
Kwa ujumla hizi ndizo faida utakazozipata
ukiifanya bizari kuwa sehemu ya viungo
katika mlo wako wa kila siku:
UTAIMARISHA KINGA YA MWILI WAKO
UTAIMARISHA AFYA YA MACHO
UTAIMARISHA SEHEMU ZA VIUNGIO VYA MWILI
WAKO
UTAIMARISHA UTENDAJI KAZI WA INI
UTAIMARISHA CHEMBE HAI ZA MWILI
UTAIMARISHA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA
UTAIMARISHA MFUMO WA DAMU MWILINI
UTASHUSHA KIWANGO CHA KOLESTRO MWILINI
UTAIMARISHA MFUMO WA UZALISHAJI MBEGU
ZA UZAZI
UTAIMARISHA KIWANGO CHA SUKARI
MWILINI.
Chapisha Maoni