MATATIZO YANAYOSABABISHA MWANAMKE ASISHIKE MIMBA

0 coment

MWANAMKE kutoshika mimba
kumegawanyika katika makundi makubwa
mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary
Infertility’ ambapo mwanamke hana historia
ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo
‘Sekondari Infertility’, hapa mwanamke
anayo historia kama alishawahi kupata
ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa au
iliharibika.
Matatizo ya kutoshika mimba kwa
mwanamke kitaalamu tunaita ‘infertility’ au
ugumba.
Kutoshika mimba kwa mwanamke
husababishwa na mambo mengi ingawa
tutakuja kuona vyanzo vikuu.
Maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni
ya lishe na magonjwa sugu pia huathiri hali
hii ya ugumba kwa mwanamke.
Chanzo cha matatizo ya ugumba kwa
mwanamke
Vyanzo vya matatizo haya vinahusisha aina
zote mbili za ugumba za ‘Primary’ na
sekondari’. Kwanza kabisa ni chanzo
kinachohusu upevushaji wa mayai
‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake
kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke
anapata siku zake kama kawaida lakini
hapevushi mayai.
Hii husababishwa na matatizo katika mfumo
wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea
lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini
au matumizi yanayohusiana na dawa za
homoni kutumika kiholela au matumizi ya
baadhi ya vyakula au vipodozi, tutakuja
kuona.
Katika makala zijazo
Dalili za upevushaji wa mayai zipo nyingi,
tutakuja kuziona hapo baadaye lakini kubwa
ni kwa mwanamke kupata ute wa uzazi
ambapo upo wa aina tatu.
Pia upevushaji tunaweza kuuona kwa
kutumia vifaa maalumu ambavyo unatumia
mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo
siku unazohisi unaweza kupata mimba.
Tatizo lingine la chanzo cha ugumba ni
kwenye mirija, mirija inaweza kuziba,
kutanuka au kuweka usaha au maji.
Maambukizi katika mirija au upasuaji wa
mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi.
Utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa
mara ukeni husababisha athari katika kizazi
na mirija. Matatizo ya mirija husababisha
ugumba kwa kiasi kikubwa ambacho ni kati
ya asilimia 15 hadi 40 kwa wanawake
ambacho ni kiwango kikubwa kuliko
matatizo mengine.
Mwanamke pia anaweza kuwa na kasoro
katika tabaka la ndani la kizazi ambapo
linatoka kwa nje badala kuwa ndani. Hali hii
kitaalam inaitwa ‘Endometriosis’. Siyo tatizo
linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini
linaathiri baadhi ya wanawake.
Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika
maumivu chini ya tumbo na huwa makali
wakati wa hedhi na kusababisha damu ya
hedhi kutoka kidogokidogo, mwanamke
hupoteza uwezo wa kushika mimba.
Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya
tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki
pia husababisha ugumba kwa mwanaume
ambao humuathiri mwanamke. Mwanaume
pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri,
anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni
tatizo kubwa.
Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi
hata kama anayo historia ya kumpa
mwanamke mimba au kuwa na watoto kwa
hiyo ni vema naye akafanyiwa uchunguzi
endapo wanatafuta mtoto au ujauzito kwa
mwaka mmoja bila ya mafanikio.
Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya
uchunguzi wa kina inaonekana mume hana
tatizo wala mke hana tatizo, hali hii inaitwa
kitaalamu ‘Unexplained Inferlity. Kwa hiyo, ni
vema uchunguzi wa kina ufanyike. Tatizo hili
tutakuja kuliona katika makala zijazo.
Uchunguzi
Matatizo ya ugumba ni makubwa na huumiza
vichwa vya watu wanaotafuta ujauzito.
Tumeona sababu kuu za ugumba lakini
mambo mengine yanayohusiana na lishe na
magonjwa sugu yanayoathiri uzazi. Tutakuja
kuzungumzia.
Uchunguzi hufanyika kwa madaktari wa
magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi
katika hospitali za mikoa na wilaya. Vipimo
mbalimbali hufanyika kama damu kuangalia
viwango vya homoni, ultrasound na mirija
uzazi.
Photo: MATATIZO YANAYOSABABISHA
MWANAMKE ASISHIKE MIMBA

Share this article :

Chapisha Maoni

Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved