KAHAWA |
Utafiti unaonyesha wanaume wanaokunywa
kahawa kwa wingi wana nafasi nzuri ya
kuepuka kensa ya tezi la kibofu cha mkojo
Kahawa ni kinywaji kikubwa katika nchi za
Afrika Mashariki kama Tanzania, Kenya...
Utafiti mpya uliofanywa kwa kushirikisha
wanaume elfu 50 unasema kuwa watu
wanaokunywa kahawa kwa wingi wana nafasi
nzuri ya kuepukana na saratani au kensa ya
tezi la kibofu cha mkojo.
Kwa muda wa zaidi ya miaka 20 kumekuwa
na imani kuwa unywaji kahawa unasaidia
katika kuepusha kensa hiyo, lakini katika tafiti
huu mpya wanasayansi wanasema
wamegundua tofauti kubwa katika kuepusha
saratani kali.
Mwanasayansi Kathryn Wilson wa Idara ya
afya ya umma ya chuo kikuu cha Havard
nchini Marekani anasema "wanaume
wanaokunywa vikombe sita au zaidi vya
kahawa kwa siku wanapunguza uwezekano
wa kupata kensa hiyo kwa asilimia 60
ukilinganisha na wanaume wasiokunywa
kabisa kahawa."
Kahawa ina kemikali mbali mbali, ikiwa na
viambatisho vinavyopambana na magonjwa
na hiyo huenda ni pamoja na kemikali
zinazozuia kensa ya tezi la kibofu cha mkojo.
Kensa hiyo ni ya pili kwa kuuwa wanaume
duniani, ikiwa inasababisha vifo vya watu
wapatao robo millioni kwa mwaka.
"wanaume wanaokunywa vikombe sita au
zaidi vya kahawa kwa siku wanapunguza
uwezekano wa kupata kensa hiyo kwa
asilimia 60 ukilinganisha na wanaume
wasiokunywa kabisa kahawa.
+ coment + 1 coment
sikio lina niuma mpaka linatoa usaa pamoua na harufu kali sana naombeni mnisaidie ndugu zangu niweke dawa gani niweze kupona maana kichwa kimeanza kuuma sana
Chapisha Maoni