Nigeria haihitaji msaada wa Vikosi vya Umoja
wa Mataifa kupambana na Boko
Haram.Mshauri wa maswala ya usalama wa
taifa nchini humo ameiambia BBC.
Sambo Dasuki amesema Nigeria na majirani zake
Niger,Chad na Cameroon wanamudu
kushughulikia swala la Wanamgambo wa
kiislamu.
Dasuki amekiri kuwa Wanamgambo ni tishio
kubwa la usalama nchini humo na kusema kuwa
takriban asilimia 50 ya Jeshi la Nigeria limepelekwa
kaskazini mashariki .
Amesema hatua hiyo inaashiria namna Jeshi
lilivyolichukulia swala hili kwa umakini mkubwa.
Alipoulizwa na Kipindi cha Newsday cha BBC kama
Nigeria inahitaji msaada wowote wa nje , alisema
''hapana''
Wanamgambo wa Boko Haram walianza
Operesheni yao mwaka 2009, wakidai kuwa
wanataka kuunda taifa la kiislamu.
Tangu Serikali ilipotangaza hali ya hatari miezi 20
iliyopita kaskazini mashariki ili kupambana na
Wanamgambo, kundi hilo limejiimarisha na sasa
linadhibiti miji kadhaa .
BBC
Chapisha Maoni