HABBAT SAWDA INATIBU KILA KITU ISIPOKUWA MAUTI -2

0 coment

Maumivu ya Kichwa
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa , karafuu
iliosagwa nusu ya kiwango cha Habbat-
Sawdaa na anisuni (anise), halafu achanganye
pamoja. Achukue kiasi cha kijiko kimoja (cha
chai), wakati wa kuumwa na kichwa, na ale na
maziwa lala (mala), pamoja na kupasugua
mahala paumapo kwa mafuta ya Habbat-
Sawdaa .

Ukosefu Wa Usingizi
Atachukua kijiko cha Habbat-Sawdaa ,
achanganye na gilasi ya maziwa moto
yaliochanganywa na asali, baada ya kupoa kiasi
atakunywa.

Chawa Na Mayai Yake
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa uliosagwa
vizuri aukande kwenye siki mpaka uwe kama
marhamu, halafu ajipake kichwani – baada ya
kunyoa nywele au kuisugua marhamu kwenye
mashina ya nywele, halafu aketi katika mwanga
wa jua kitambo cha robo-saa. Na hataosha
kichwa ela baada ya masaa matano. Atafanya
hivyo kila siku kwa muda wa wiki moja.

Kisunzi Na Maumivu Ya Sikio
Tone moja la mafuta ya Habbat-Sawdaa ndani
ya sikio husafisha sikio, pamoja na kuyanywa
na kusugua sehemu za panda na nyuma ya
kichwa, humaliza kisunzi.

Upaa Na Mabaka
Utachukua kijiko cha unga wa Habbat-Sawdaa,
siki kiasi cha kikombe kimoja na juisi ya
kitunguu saumu kiasi cha kijiko kidogo, vyote
hivyo utavichanganya na vitakua namna ya
marhamu, utajipaka baada ya kunyoa sehemu
ya nywele na kuchanja kidogo – kisha utafunga
bendeji, utaiacha mpaka asubuhi, baadae
utajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa,utaendelea
hivyo kwa muda wa wiki moja.

Malengelenge ya Neva katika Ngozi
Atajipaka – sehemu ya malengelenge – mafuta
ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku mpaka
iondoke kwa Uwezo wa Allah.

Maradhi Ya Wanawake Na Uzazi
Dawa kubwa inayosahilisha kuzaa ni Habbat-
Sawdaa iliochemshwa ikachanganywa na asali
na kiziduo cha babunaji (chamomile). H abat
sawdaa ni kama burashi katika uke wa
mwanamke yenye faida kubwa kwao pamoja
na kutumua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika
kila kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya
wanawake.

Meno Na Maumivu Ya Mafido na Koo
Kiziduo cha Habbat-Sawdaa na kutumia kwa
kusukutua kwa kugogomoa, husaidia mno
maradhi yote ya mdomo na koo, vivyo hivyo
pamoja na kubugia kijiko cha Habbat-Sawdaa
na kumeza kwa maji yenye vuguvugu kila siku
na kujipaka mafuta yake sehemu ya koo kwa
nje na kuusugua ufizi kwa ndani.

Maradhi Ya Tezi
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa na
aukande kwa asali na mkate wa nyuki kila siku,
kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Chunusi (Acne)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande
katika mafuta ya ufuta (simsimu) pamoja na
kijiko cha unga wa ngano. Vyote hivyo
atajipaka usoni kuanzia jioni hadi asubuhi,
halafu ataosha kwa maji yenye vuguvugu kwa
sabuni. Ataendelea kufanya hivyo kwa muda
wa wiki moja. Na awe akinywa mafuta ya
Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha
moto.

Maradhi Yote ya Ngozi
Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta
ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano
asili, vyote hivyo kwa viwango sawa, ule unga
wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu
aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse
sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa
kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi
kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku.
Lakini ajizuie na kila chenye kuchochea hisia
kama vile, samaki, mayai, maembe na mfano
wake.

Sugu (Chunjua) (Wart)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande
katika siki nzito na asugue kwa kitambaa cha
sufi au katani mahala pa sugu asubuhi na jioni
kwa muda wa wiki moja.
Kuung`arisha Uso Na Kuurembesha
Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika
mafuta ya zeituni, na atajipaka usoni halafu
apigwe na mwanga wa jua kidogo. Tiba hiyo
ataifanya wakati wowote katika mchana na
siku yoyote.

Kuunganisha Mvunjiko Haraka
Supu ya adesi (dengu), kitunguu maji pamoja
na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha
unga wa Habbat-Sawdaa , utachanganya na
supu hiyo japo siku baada ya siku; halafu
anywe. Na atasugua sehemu zilizo karibu na
mvunjiko kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa, na
baada ya kufungua bendeji atajisugua kwa
mafuta ya Habbat-Sawdaa yenye vuguvugu;
kila siku.

Mvilio Wa Damu (Contusion)
Atachemsha vizuri konde moja la Habbat-
Sawdaa katika chombo cha maji, kisha
atakiingiza kiungo kilichovilia damu ndani ya
maji hayo- yenye vuguvugu- kwa muda wa
robo-saa au zaidi pamoja na kukitaharakisha
kiungo hicho. Baada ya hapo atajipaka mafuta
ya Habbat-Sawdaa bila ya kufunga kitu. Lakini
hatakiwi kukipa uzito kiungo hicho au
kukitaabisha. Tiba hiyo ataifanya kila siku kabla
ya kulala.

Baridi Yabisi (Rheumatism)
Atachemsha mafuta ya Habbat-Sawdaa na
atasugua kwayo ile sehemu yenye ugonjwa,
atasugua kwa nguvu kama kwamba
yuwasugua mfupa wala sio ngozi! Na
atayanywa baada ya kuyachemsha vyema na
kuyachanganya na asali kidogo. Ataendelea na
tiba hiyo huku akiwa ni mwenye imani na
yakini kuwa Allah Atamponya.

(Ki) Sukari (Diabetes)
Utachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha
kikombe kimoja, manemane (myrrh) iliosagwa
kiasi cha kijiko kikubwa, habbarrashad nusu
kikombe, komamanga iliosagwa kiasi cha
kikombe kimoja, mzizi wa kabichi uliosagwa
baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja
na kijiko kidogo cha mvuje. Vyote hivyo
atavichanganya na atakula kabla ya kula
chakula kiasi cha kijiko kimoja, atakula na
maziwa lala ili iwe rahisi kumeza.
Shinikizo la Damu (High Blood)
Kila unywapo kinywaji cha moto, tia matone
machache ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Pia
ujipake mafuta hayo mwili wote, japo wiki mara
moja.

Uvimbe Wa Figo(Nephritis)
Atatengeneza kibandiko (cha kitambaa)
kutokana na unga wa Habbat-Sawdaa
uliokandwa katika mafuta ya zeituni,
atabandika sehemu yenye maumivu ya figo
pamoja na kubugia funda la kijiko cha Habbat-
Sawdaa kila siku kabla ya kula chakula kwa
muda wa wiki moja tu; uvimbe utakwisha insha
Allah.

Kuvunjavunja Vijiwe Vya Tumboni
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha
kikombe kimoja kisha aukande katika kikombe
cha asali, na atasaga kitungu u saumu punje
tatu; atakua akichukua nusu yake akila kabla
ya kula chakula kila siku. Pia itakua bora lau
atakula limau kila baada ya kula dawa; kwani
husafisha kabisa.

Kukojoa Kwa Maumivu (Dysuria)
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa juu ya
kinena kabla ya kulala pamoja na kunywa
kikombe cha mafuta hayo yaliochemshwa na
kutiwa asali; kila siku kabla ya kulala.

Kukojoa Bila Kukusudia
Atachukua Habbat-Sawdaa na maganda ya
mayai yaliosafishwa na yakaokwa na kusagwa
halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa
kisha yakaokwa na kusagwa halafu
yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha
aingize kwenye maziwa; hatimae anywe kiasi
cha kikombe kimoja kila siku na wakati
wowote.

Jongo (Edema)
Ataweka kibandiko (cha kitambaa) cha unga
wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika siki juu
ya kitovu, kwanza ataweka kitambaa. Pia
atakula Habbat-Sawdaa kijiko kimoja asubuhi
na jioni kwa muda wa wiki moja.

Kifuko Cha Nyongo Na Vijiwe Vyake
Atachukua Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko
kimoja, manemane iliosagwa robo kijiko na
asali kiasi cha kikombe kimoja; vyote hivyo
atavichanganya viwe mraba (kama jamu);
halafu awe akila kila asubuhi na jioni.

Wengu
Ataweka kibandiko (kilichopashwa moto) cha
Habbat-Sawdaa iliokandwa katika mafuta ya
zeti katika ubavu wa kushoto; jioni. Na wakati
huo huo ata kunywa kikombe cha kiziduo cha
uwatu kilichochanganywa asali na mafuta ya
Habbat-Sawdaa kidogo, ataendalea na dawa
hiyo kwa muda wa wiki mbili mfululizo.
Maradhi Yote ya Kifua na Baridi
Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa kiasi cha
kijiko kikubwa atie kwenye maji halafu
ayaweke juu ya moto mpaka ianze kufuka
moshi, hapo aanze kuuvuta ule moshi puani
huku akiwa amejifunika kichwa ili ule moshi
usiende upande mwingine. Atafanya hivyo kila
siku kabla ya kulala, pamoja na kunywa kiziduo
cha zaatari kilichochanganywa na unga wa
Habbat-Sawdaa; asubuhi na jioni.
Moyo na Mzungukoa wa Damu
Kuwa na imani katika maneno ya Mtume (Swalla
Llahu ‘alayhi wa sallam) Kwa sababu jambo hili
ni katika muktadha wa imani. Mtume (Swalla
Llahu ‘alayhi wa sallam) alipotuambia kuwa
Habbat-Sawdaa ni dawa ya kila ugonjwa, basi
hakuna shaka hata chembe kuwa ni dawa ya
maradhi yote yanayomfika mwanaaadamu.
Mgonjwa wa moyo asikate tamaa kutokana na
rehma ya Allah; ni juu yake akithirishe kutumia
Habbat-Sawdaa kwa namna yoyote iwayo; iwe
ni kwa kula nzima au kwa kunywa wakati
wowote uwao.

Mchango (Msokoto Wa Tumbo) (Colic)
Atachemsha vyema anisuni, kamun na nana
kwa vipimo sawa na atatia asali kidogo, halafu
atie matone saba ya Habbat-Sawdaa ;
atakunywa kinywaji hicho kikiwa na vuguvugu
pamoja na kupaka mafuta ya Habbat-Sawdaa
mahala panaposokota. Baada ya muda
mchache maumivu yataondoka.

Kuhara
Atachukua juisi ya chirichiri iliochanganywa na
unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kikumbwa,
atakunywa kiasi cha kikombe kimoja mara tatu
kwa siku.

Uziwi
Atachemsha Habbat-Sawdaa pamoja na
karafuu, na atakunywa bila ya kuongeza kitu;
mara tatu kwa siku.

Gesi Na Maumivu
Atabugia unga laini wa Habbat-Sawdaa kiasi
cha kijiko kimoja kabla ya kula chakula
akifwatisha gilasi ya maji yenye vuguvugu
iliotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu;
atakariri kila siku kwa muda wa wiki moja
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved