Katibu mtendaji wa baraza la maimamu na
wahubiri nchini Kenya CIPK Sheikh Mohamed
Khalifa amedinda kujibu shutma zinazokabili
baraza hilo kuhusiana na mzozo wa uchaguzi
katika tawi la baraza hilo Pwani Kusini.
Katika mahojiano Sheikh Khalifa amesema hana
muda wa kuangazia mzozo huo wa uchaguzi hasa
baada ya kubainika kuna upinzani baina ya
kamati ya sasa na ile iliyopita.
Duru kutoka Pwani Kusini zimearifu kwamba
uteuzi huo ulifanywa ili kuiondoa mamlakani
kamati iliyokuwepo kwa kuwa ilikinzana na
kamati kuu inayounga mkono serikali ya Jubilee
huku ile ya pwani kusini ikiunga mkono mrengo
pinzani.
Aidha kuhusiana na wakenya wanaozuiliwa
nchini Uganda kwa tuhuma za ugaidi, Sheikh
Khalifa amesema kuwa baraza hilo lilifanya kila
liwezalo kuwaokoa wakenya hao, ila kwa sasa
juhudi zao zimegonga mwamba.
Chapisha Maoni