LUGHA ZA KIGENI OFISINI MARUFUKU NCHINI SOMALIA

0 coment


Rais wa Somalia amepiga marufuku ya
matumizi ya lugha za kigeni katika ofisi za
serikali na kusema kuwa lugha pekee ya
mawasiliano katika ofisi hizo ni kisomali.
Raisi Hassan Shaykh Mahmud alikuwa
akizungumza hayo katika sherehe za maadhimisho
ya kutimiza miaka 42 tangu kuanza kutumika kwa
lugha ya Kisomali nchini humo ,maadhimisho
yaliyofanywa mjini Mogadishu kwa lengo la kutaka
kuiimarisha lugha hiyo.Hata hivyo maadhimisho
hayo yalihudhuriwa na mamabalozi
wanaowakilisha nchi zao nchini humo.
Matumizi ya lugha ya kisomali katika ofisi za serikali
yametakiwa kuanza January mosi mwaka huu na
kuendelea.Shughuli zote za kiserikali nchini humo
zimetakiwa kuendeshwa katika lugha ya kisomali
na si lugha ingine yoyote.Ruhusa ya matumizi ya
lugha za kigeni imetolewa tu wakati wageni
kutoka nje ya somalia watakapo kuwa
wakihudumiwa .
Hata hivyo waziri wa habari wa taifa hilo,ametilia
mkazo kauli hiyo na kudai kwamba January 21 ni
siku muhimu sana kwa taifa hilo,na siku hiyo ni
kumbu kumbu kwa gazeti la kisomali la kwanza
kuchapishwa.naye spika wa bunge la
Somalia,Muhammad Shaykh Usman Jawari,ambaye
pia alitoa kauli yake kwenye maadhimisho hayo,na
kusema kwamba ni jambo muhimu kwa jamii ya
wasomali kuelewa umuhimu wa lugha yao na
kuitaka jamii kuiimarisha lugha hiyo.
Rais Mahmud aliongeza kusema kwamba tarehe 21
January ni siku muhimu kwa wasomali na serikali
yao.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved