Toka kwa Mtume (S.A.W) amesema, “ Hakuna ugonjwa wowote isipokuwa katika haba soda kuna kupona kwake isipokuwa mauti.”

UKWELI WA KISAYANSI:

          Haba soda imetumika katika nchi nyingi za mashariki ya kati na ya mbali kama ni matibabu ya kienyeji tokea zaidi ya miaka elfu mbili na ikawezekana kutolewa mkusanyiko wa dawa uitwao Negelon kutokana na mafuta ya haba soda mwaka 1959 na Al Dakhani na wenzake. Mbegu ya haba soda  ina 40% ya mafuta thabiti katika uzito wake  Toka kwa Mtume (S.A.W) amesema, “ Hakuna ugonjwa wowote isipokuwa katika haba soda kuna kupona kwake isipokuwa mauti.”

UKWELI WA KISAYANSI:

          Haba soda imetumika katika nchi nyingi za mashariki ya kati na ya mbali kama ni matibabu ya kienyeji tokea zaidi ya miaka elfu mbili na ikawezekana kutolewa mkusanyiko wa dawa uitwao Negelon kutokana na mafuta ya haba soda mwaka 1959 na Al Dakhani na wenzake. Mbegu ya haba soda  ina 40% ya mafuta thabiti katika uzito wake, 1.4% mafuta mepesi na ina asidi kumi na tano, protini, kalsiamu, chuma, sodiamu, na chokaa. Na kati ya madawa yake yenye ufanisi ni : Themokenon, Dithemokenon, Themohydrokenon na Themol. Mchango wa haba soda katika kinga ya kimaumbile haukudhihirika hadi mwaka 1986 kupitia  tafiti zilizofanywa na Dk. Al - Kadhi na wenzake nchini Marekani. Kisha baaada ya hapo zikafuatia tafiti katika nchi mbalimbali na katika nyanja nyingi kuhusu mti huo. Al - Kadi amethibitisha kuwa haba soda ina athari zenye kutoa nguvu kwa kazi za kinga. Kwani kimezidi kiwango cha (Seli za limfu)  zenye kusaidia na kuwa (Seli rejea zenye kuzuia) kufikia 72% kwa wastani. Pia imeboreka harakati ya seli  za kimaumbile zenye kuua  kwa kiwango cha 74% kwa wastani. Matokeo ya baadhi ya chunguzi mpya yamekuja kuthibitisha matokeo ya tafiti za Al - Kadhi. Kati ya hayo ni:

 Yale yaliyochapishwa na jarida la kinga ya dawa katika toleo la mwezi Agosti 1995 kuhusu athari za haba soda kwa (Seli za limfu za kibinadamu) nje juu ya michupo kadhaa na juu ya harakati za kohozi  la seli nyeupe za damu zenye viini vingi. Pia utafiti uliochapishwa na jarida la kinga ya dawa katika toleo la mwezi wa Septemba mwaka 2000 AD (10) kuhusu athari za kinga za mafuta ya haba soda dhidi ya kupatwa na virusi vyenye kukuza seli ( cytomegalovirus)  katika panya. Mafuta ya haba soda yalipofanyiwa majaribio kama ni kiua virusi na hasa seli za kimaumbile zenye kuua, seli kubwa za kohozi na zoezi la kufanyika kohozi. Pia yaliyochapishwa na jarida la saratani la Ulaya katika toleo la Oktoba mwaka 1999 kuhusu athari za mkusanyiko wa Themokenon katika tumbo la panya. Pia yaliyochapishwa na jarida la tafiti za dawa za saratani katika toleo la Mei 1998 kutokana na mada za haba soda kama ni dawa ya kumalizana na saratani. Kadhalika yaliyochapishwa na jarida la Athno la madawa katika toleo la Aprili 2000 kuhusu athari za sumu na kinga kutokana na dawa ya Ethanol kutokana na mbegu za haba soda. Pia yaliyochapishwa na jarida la mimea ya tiba katika toleo la mwezi wa Februari mwaka 1995 kuhusu athari za mafuta thabiti ya haba soda  na mpangilio wa Themokenon kwa vipira vyeupe vya damu, na tafiti nyengine mbali mbali katika uwanja huo.

UPANDE WA MIUJIZA:

           Mtume (S.A.W) amesema kuwa katika haba soda kuna matibabu ya kila ugonjwa. Katika mtiririko wa hadithi zote, neno ugonjwa halikuainishwa na limekuja katika mtiririko wa kuthibitisha, kwa hiyo tunaweza kusema kuwa katika haba soda kuna sehemu ya kupona kwa kila ugonjwa. Na imethibiti kuwa chombo cha kinga mwilini ndio mpango pekee wenye kumiliki silaha maalumu ya kumalizana na kila ugonjwa, kwa kina mpango wa kinga ya kipekee au ya kimaumbile yenye kumiliki ufanyaji wa viuavijasumu maalumu kwa kila kiumbe chenye kusababisha maradhi na kuunda silaha ya seli maalumu zenye kuua.

          Imethibitika kupitia tafiti za kivitendo kuwa haba soda huchangamsha kinga ya kipekee. Kimepanda kiwango cha seli zenye kusaidia, na seli zenye kuzuia, na seli za kimaumbile zenye kuua. Nazo zote ni ( Seli za limfu) zenye kuhusika zaidi na zenye ufanisi, kwa kiasi cha 75% katika utafiti wa Al-Kadhi. Tafiti zilizochapishwa katika machapisho ya kisayansi zimethibitisha ukweli huu, kwani zimeboreka ( Seli za limfu ) zenye kusaidia na seli za kohozi. Pia umezidi mkusanyiko wa Enterveron na Enterloken 1,2 na kuboreka kinga ya seli. Ubora huo umedhihirika katika chombo cha kinga kwa athari yenye kuangamiza kwa dawa ya haba soda kwa seli za saratani na baadhi ya virusi. Pia kuboreka athari za ugonjwa wa michango ya Bilharzia. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa katika haba soda mna dawa ya kila ugonjwa, na inatendeana na kila chenye kusababisha maradhi na inamiliki utoaji wa kupona kamili au sehemu ya kila maradhi.

         Kama hivi umetukuka ukweli wa kisayansi katika hadithi hizi tukufu ambazo hakuna hata mtu mmoja aliyeweza kuzidiriki  mbali ya kuzisema tu na kuwazungumzia watu tokea karne kumi na nne isipokuwa Mtume (S.A.W) aliyetumwa na Mwenyezi Mungu. Amesema kweli Mwenyezi Mungu aliyesema, “ Na wala hasemi kwa matamanio  (ya nafsi yake). Hayakuwa (haya anayoyasema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake).” Suratu Nnajmi aya za 3 – 4.