Asali |
mwonyeshaji mitindo ya mavazi na muigizaji sinema Jocqol Bell."
Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na
magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama
itachanganywa na mdalasini wa kawaida.
Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa
yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za
umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.
Kama ifuatayo:
1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali
pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua
sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.
Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya
asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.
Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa
wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila
asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na _
ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.
2. kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo
maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu
unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.
3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu
zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha
kwenye kipindi cha wiki moja.
4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja
{cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya
maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.
5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.
6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry
nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.
7. Helemu {CHOLESTERAL}
Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia
10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili
vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi
nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini.
Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara
ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric
Vogelmann.
Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. vilevile/ aidha
uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya
helemu.
> 8. Mafua {COLDS}
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika
kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha
mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.
9. Ugumba {INFERTILITY}
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa anglao vijiko
viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}. \
Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi
ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.
Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa
kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.
Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike
baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto
hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.
10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na
kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu
yaletwayo na vidonda vya tumbo.
ll.Esidi/Gesi-Co2. Hco3. Hcl.
Kula asali pamoja na mdalasini huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi/acid
kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi iliofanywa huko India na Japan.
12.Ugonjwa wa Moyo {HEART DISEASE}
Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye
mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara-kwa kupakaa wakati wa kifiingua kinywa.
Kula asali ya mkate wa ngano yenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko kimoja {cha mezani} cha
mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Tiba hii ya maajabu iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya
damu kwa 74% ya wagonjwa waliokuwa katika nyumba za kutunzia wagonjwa - utafiti mmoja
ulionyesha.
13. Shinikizo la damu {HIGH BLOOD PRESSURE}
Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo ya maumivu ya kifua na kizunguzungu
yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa kitaliano kuwapa dozi za
mara kwa mara za asali ilyochanganywa na mdalasini. Vipimo vya shinikizo la damu vilionyesha
ukawaida na wote 137 waliofanyiwa jaribio hilo waliripoti kujisikia vyema/vizuri baada ya wiki chache za
tiba hii ya ajabu.
14.Kinga ya mwili {IMMUNE SYSTEM}
Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa
pamoja - wataalamu wanasema.
Utafiti wa kitiba unaonyesha kwamba hazina kubwa ya vitamini{vivurutubisho}na madini pamoja na
michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za
damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea {virus} na {bacteria}.
15.Ukosefu wa nguvu za kiume [Uhanithi]{IMPOTENCE}
Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi.
Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya
dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana, watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo
wa kupeleka mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa na dunia ya
kusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao
za kufanya mapenzi.
16.Kutokuchaguliwa kwa chakula {INDIGESTION}
Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo{kula chakula} huondoa kiungulia na
wataalamu wanasema kwamba asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa vyakula
tumboni na mdalasini unaongeza spidi ya kuchaguliwa kwa vyakula.
17.Flu {INFLTJENZA}
Tafiti moja ya kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu
vairasi {vimelea} waletayo Flu.
18.Umri wa kuishi {LONGERVITY}
Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila
siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko
vine{vikubwa} vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10. kunywa robo
kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
19.Chunusi {PIMPLES}
Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bacteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.
20.Kuumwa na wadudu {kwa washawasha} wenye sumu
Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwahso
unapokuathiri. Rudia tena hadi viuvimbe vinatoweka.
21.Madhara ya ngozi {INFECTIONS}
Fanya kama ilivyoelekezwa hapo juu. Rudia kufanya hivyo hadi hali itakapokwisha.
22.Kupungua kwa uzito
Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili
ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili
ambavyo ni asali na mdalasini.unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika
mapishi yako. Vilevile, wataalamu wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje
ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na kijiko kimoja cha
mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu. Rudia mchanganyiko huu kabla ya kulala.
Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana na mazoezi machache, kuongeza
hivi vitu viwili vya asili katika chakula ni muafaka. Pia kinywaji hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na
wataalamu wa lishe kwamba hupunguza hamu ya kula pamoja na kuleta joto mwilini.
23.Sarakani {CANCER}
Utafiti uliomalizika karibuni huko Australia na Japan, umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa
katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu sarakani.
Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa sarakani ya
mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionyesha maradufu
kupata nafuu kuliko wale waliokuwa wakitumia wakitumia madawa ya sarakani pekee. "Tuliwapa kijiko
cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi".anasema Dr Hiroki Owatta. "Wengine waliendelea na
milo ya kawaida".
24.Uchovu {FATIGUE}
Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali zina uwezo wa kuongeza nishati
mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na
uchovu, wataalamu wanapendekeza kuchauganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji,
nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9 alasiri
wakati nishati {nguvu}inapoanza kushuka" anashauri Dr Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali
na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa. "katika wiki moja hii
itajionyesha".
25.Kuvimba Nyayo {SORE FEET}
Chua asali na mdalasini vuguvugu katika {miguu} nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au
baada ya mazoezi marefu. Rudia kila asubuhi halafu nawisha nyayo kwenye maji baridi na vaa viatu.
26.Harufu mbaya kutoka mdomoni
Waamerica wa kusini wanasukutua kwa kutumia asali na mdalasini pamoja na vuguvugu kila asubuhi
ili kufanya harufu toka mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya kusini mashariki, watu hula
kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni {halitosis}. Wataalamu wanaamini
kwamba uwezo wa kuua bacteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo
mdomoni.
27.Kupungua kwa usikivu {HEARING LOSS}
Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na
Wagiriki wa zamani.
Chapisha Maoni