HOSPITALI YA MBEYA YATEULIWA KUPIMA EBOLA

0 coment


Hospitali ya Rufaa Mbeya (MRH), imeteuliwa rasmi
kuwa na maabara maalumu ya kuwapima watu
watakaohisiwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa
ebola.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Mpoki
Ulisubisya alisema hayo jana jioni alipozungumza
mambo mbalimbali kuhusu changamoto
zinazoikabili hospitali yake.
"Ni kweli Serikali imeiteua maabara yetu ya
hospitali kuwa maabara maalumu ya kupima virusi
vya ebola nchini na kwa sasa maandalizi yote
yanakamilishwa na tutaanza kazi mwishoni mwa
mwezi huu au mapema Februari’’ alisema.
Kwa kipindi cha miaka mitano sasa, Maabara ya
Hospitali ya Rufaa Mbeya ni maabara ambayo
imethibitishwa kimataifa kwa ubora na kwamba
vipimo vikitolewa kwenye maabara hiyo
vinakubalika hata nchi za Marekani na Uingereza.
Akizungumzia uboreshaji wa utendaji kazi
amesema wafanyakazi kupitia kwa viongozi wao
kwa sasa wameimarisha utendaji kazi.
Kuhusu chumba cha kuhifadhi maiti kwenye
Hospitali hiyo, Ulisubisya amesema Serikali
imempata mtu atakayejenga jengo kubwa la
kuhifadhi maiti na kuliboresha ili kuendeshwa
kwa ubia katika hali ya usafi na kisasa zaidi.
‘’Bila shaka unakumbuka , mfanyakazi wa chumba
cha maiti aliwahi kumweleza Waziri kwamba
ukifariki dunia ukiwa Mbeya maiti yako italazwa
chini. Sasa Serikali imeamua kuchukua hatua ili
kuboresha nyumba hizo ingawa wahusika
watatakiwa kutoa mchango kidogo’’alisema.
Mapema mwaka jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii Dk Seif Rashid wakati huo akiwa Naibu
Waziri alitembelea hospitali hiyo ambapo
mfanyakazi wa Chumba cha maiti, Vuruga P
Vuruga alimweleza kiongozi huyo kwamba maiti
zinalazwa mbili mbili kwenye chumba chenye
uwezo wa kuhifadhi watu sita.
Vuruga amesema kutokana na kasi ya kufa, hivi
sasa maiti zinalazwa chini na kwamba hata Naibu
Waziri angefariki akiwa Mbeya ajue maiti yake
ingelazwa chini

MWANANCHI.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved