WENYEVITI wa Kamati za Kudumu za Bunge,
waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo
katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow,
wamejiuzulu nyadhifa zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Spika Anne
Makinda aliwaambia waandishi wa habari katika
Ofisi ndogo ya Bunge, waliotaka kujua hatima ya
wenyeviti hao, kuwa hawapo tena katika nafasi
zao baada ya kujiuzulu.
“Wenyeviti hao kwa ninavyojua mimi wamejiuzulu,
kama ambavyo azimio lilivyotaka, kama wapo hizo
taarifa mimi sina na sijui kinachoendelea,
nawaambia mimi wameshajiuzulu,” alisema Spika
Makinda.
Makinda alisema wenyeviti hao, ambao ni wa
Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa,
wa Katiba, Sheria na Utawala William Ngeleja na
Andrew Chenge wa Kamati ya Bajeti, hawaendelei
tena na nafasi zao, kupisha viongozi wengine
kuchaguliwa ndani ya kamati husika.
Hata hivyo, Makinda alipoulizwa kama wenyeviti
hao kama wamejiuzulu rasmi kwa barua na kama
yeye amezipokea lini, alisema viongozi hao ni wa
kamati na hivyo wamewajibika katika kamati zao.
“Mimi ndiye Spika, nasema wamejiuzulu… msiniulize
barua zao wala nini, heshima ya mtu ni kujiuzulu
mwenyewe bwana na wao wamefanya hivyo,”
alisema Spika Makinda.
Katika Azimio namba tatu la Bunge katika
majadiliano ya sakata hilo, Bunge lilielekeza kuwa
kamati husika za kudumu za Bunge, zichukue
hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya
mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao
wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za
Bunge.
Utekelezaji wa azimio hilo, unakuja baada ya
Serikali kutekeleza maagizo ya Bunge hilo kwa
kuwawajibisha baadhi ya viongozi wake,
waliotajwa katika ripoti hiyo.
Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi
(CCM), alitajwa katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC) kuwa aliwekewa Sh bilioni
1.6 katika akaunti yake binafsi na Ngejela ambaye
ni Mbunge wa Sengerema (CCM) aliingiziwa Sh
milioni 40.4 kwenye akaunti.
Waliingiziwa fedha hizo na mmiliki wa Kampuni ya
VIP Engineering & Marketing, James Rugemalira.
Mwambalaswa ambaye pia ni Mbunge wa Lupa
(CCM), ametajwa kuwa alikuwa Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme nchini
(TANESCO), ambayo Bunge liliazimia kuwa
wajumbe wake wote wawajibishwe.
Katika utekelezaji wa maazimio hayo, Rais Jakaya
Kikwete alimtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
kupisha katika nafasi hiyo ili ateuliwe mtu
mwingine na tayari Profesa huyo ameshapisha.
Profesa Tibaijuka aliingiziwa Sh bilioni 1.6 katika
akaunti yake binafsi, kinyume na kanuni za maadili
ya viongozi wa umma.
Rais Kikwete pia alimweka kiporo Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi
amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa
tuhuma dhidi yake.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema, alishajiuzulu.
HABARI LEO

Chapisha Maoni