Mfalme wa Saudi Arabia na Mhudumu wa Misikiti
miwili mitakatifu amefariki dunia akiwa hospitalini
televisheni ya Taifa ya nchi hiyo imetangaza.
Tamko la kifo cha mfalme huyo zilitolewa na kaka
wa mfalme huyo aitwaye, Salman ambaye naye
aliwahi kuwa mfalme.
Kabla ya tamko hilo televisheni ya taifa la Saudi
lilikatiza matangazo yake na kuweka Quraan,kama
ishara ya kifo cha kiongozi wa juu wa ufalme.
Mfalme Abdullah, amefariki dunia akiwa na miaka
90, alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa tangu
Desemba mwaka wa jana kutokana na homa ya
mapafu 'pneumonia' (Nimonia).
Mfalme huyo aliingia madarakani mwaka 2005
kuchukua nafasi hiyo kufuatia kifo cha Mfalme
Fahdi lakini alikuwa ni dhaifu mwenye
kushambuliwa na maradhi mara kwa mara.
Taarifa zinasema Mfalme alifariki saa nne za usiku
wa kuamkia ijumaa na anatarajiwa kuzikwa leo
mchana.
Nafasi ya ufalme kwa sasa itakuwa kwa Prince
Salman mwenye umri wa miaka 79.
Chapisha Maoni