Amesema Fadhwyl Ibn ‘Iyaadh (Rahimahu Allah) : “ Nimejifunza subra kutoka kwa mtoto mdogo. Siku moja nilikwenda msikitini. Nikamuona mwanamke kutoka ndani ya nyumba yake akimpiga mwanawe. Mtoto alikuwa akilia kwa kelele. Yule mwanamke akatoka nje na akamfungia mlango mtoto ndani ya nyumba.
Akasema Fadhwyl niliporejea kutoka msikitini, nikapita kwenye ile nyumba kumtizama yule mtoto, nikamkuta yule mtoto baada ya kidogo kumaliza kulia amekaa chini ya mlango akimbembeleza mama yake na kumuomba msamaha. Moyo wa mama ukalainika na akamfungulia mlango.”
Fadhwyl alilia sana mpaka ndevu zake zikajaa machozi. Mwisho akasema “ Subhana Allah!! Lau mja angelikuwa mwenye kusubiri katika milango ya Allah basi Allah angemfungulia”
Amesema Abu Dardai (Radhi za Allah ziwe juu yake) :" Jitahidini katika kuomba dua kwani hakika mwenye kugonga mlango sana huwa karibu kufunguliwa"
Na sisi tusiache kusubiri katika milango ya Allah (subhanahu wataala) kwa subra na kwa dua zetu kwake. Dua ambazo kwa hakika Allah (subhanahu wataala) kwa anazikubali
Chapisha Maoni