MATUMIZI ya mafuta ya habat soda ni mengi
sana katika mwili wa binadamu lakini leo
utajifunza na kufaidika na haya machache
ambayo ninayaandika hapa chini:
KWA AFYA
Kunywa kijiko kimoja cha mafuta haya
asubuhi na usiku, tena asubuhi unaweza
kunywa kabla ya kifungua kinywa. Unaweza
kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake
au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali
safi.
HAMU YA KULA
Kabla ya kuanza kula, jipatie kijiko kimoja cha
mafuta hayo kisha kunywa maji ya kawaida
au yaliyochanganywa na siki kidogo.
VIPELE, CHUNUSI NA NGOZI
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili
kikombe kimoja cha habat soda iliyosagwa,
½ (nusu) kikombe cha maganda ya
komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu)
kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi
ya tufaha (apple). Paka sehemu inayotakiwa
kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka
vipele (chunusi) vitakapoondoka.
Mchanganyiko huu unaweza kukaa mpaka
wiki tatu, ni lazima uuweke katika hali ya
baridi.
PUMU
Weka kijiko cha habat soda iliyochemshwa
katika maji yaliyochemshwa kisha unywe
ikiwa ya moto.
KUTIBU MGONGO
(sehemu ya chini)
Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko
cha habat soda kunywa kabla hujala kitu
chochote wakati wa asubuhi.
KIBOFU/FIGO
Kama unasumbuliwa na kibofu cha mkojo au
figo, tumia asali kila asubuhi kabla ya
kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili
vya habat soda iliyosagwa na ½ (nusu)
kikombe cha asali safi.
Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko
huu pamoja na kikombe kimoja cha maji ya
moto kila asubuhi kabla ya kufungua
kinywa. Mchanganyiko wa asali na habat
soda unaweza kukaa kwa siku 15 tu na
hifadhi kwenye baridi.
KIKOHOZI
Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya
habat soda kwenye kahawa au chai.
Kunywa kijiko kimoja cha habat soda na asali
mchana na usiku. Pia kwa wenye matatizo ya
kutokwa na haja ndogo (mkojo): Kunywa
kijiko kimoja cha habat soda pamoja na asali,
kisha kunywa maji ya uvuguvugu.
NGOZI KAVU
Kwa wale wenye ngozi kavu changanya asali
pamoja na robo kijiko cha mafuta ya habat
soda, kunywa wakati wa asubuhi kabla ya
kufungua kinywa.
MINYOO:
Kunywa habat soda pamoja na siki kuondoa
minyoo ya aina yoyote ile, inaweza kuwa ya
limao au ya tufaha ‘apple’.
KICHWA
Kama unasumbuliwa na kichwa, chukua
unga wa habat soda, karafuu iliyosagwa
nusu, kijiko cha habat sauda kisha
uchanganye.
chukua kijiko kimoja cha chai kisha kunywa
na mafuta yake unaweza kupaka kichwani.
USINGIZI
Kama una tatizo la kukosa usingizi, chukua
kijiko kimoja cha habat soda changanya na
maziwa glasi moja pamoja na asali kijiko
kimoja kikubwa kisha kunywa.
SIKIO
Chukua tone moja la mafuta ya habat soda
nyunyizia ndani ya sikio husaidia kulisafisha
na kuliponya kabisa.
MALENGELENGE
Chukua mafuta ya habat soda jipake mpaka
yaishe.
MARADHI YA WANAWAKE
Tumia mafuta ya habat soda, kunywa
kwenye kila kinywaji cha moto, unaweza
kuweka kijiko kimoja kwenye maziwa,
kwenye maji ya moto, kwenye supu n.k.
Mbali na matatizo hayo pia inasaidia kusafisha
kizazi na ni rahisi kwa mwanamke asiyezaa
kushika mimba kwa haraka.
KUSIKIA VIZURI
Mtu mwenye ugonjwa wa kutosikia
achemshe habat soda na karafuu, anywe bila
kuongeza kitu chochote mara tatu kwa siku
atapona.
VIDONDA
Kama una kidonda changanya matone kumi
ya mafuta ya habat soda katika kikombe cha
asali na kijiko kimoja cha maganda ya
komamanga yaliyokaushwa na kusagwa.
Kula mchanganyiko huu kabla ya kula
chakula baadaye kunywa glasi ya maziwa
yasiyotiwa kitu chochote.
Chapisha Maoni