KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI

0 coment



Kuziba kwa mirija ya uzazi ya mwanamke ni
tatizo kubwa na ndiyo linaloongoza
kusababisha ugumba kwa mwanamke
ingawa hata matatizo ya vichecheo au
homoni pia huchangia.Wanawake wengi
wanaohangaika kutafuta watoto
hugundulika na tatizo la mirija kuziba.

Matatizo ya mirija ya uzazi kwa wanawake
yapo wengi, mfano mirija inaweza kuvimba
na kupoteza uhalisia hivyo kushindwa
kutungisha mimba. Mirija inaweza kujaa
usaha au maji. Tatizo hili ni kubwa lakini
ukifuatilia utakuta linaweza kuzuilika.
Kuziba kwa mirija ni athari za matatizo katika
kizazi.

Jinsi tatizo linavyotokea
Matatizo katika mfumo wa uzazi huanzia
aidha ukeni au ndani ya kizazi. Maambukizi
ya ukeni huweza kujipenyeza hadi ndani ya
kizazi na kushambulia tabaka la ndani ya
kizazi na mirija.

Maambukizi yanayoanzia ndani ya kizazi pia
husambaa hadi ndani ya mirija. Mirija
hushambuliwa kwa ndani na nje ya kizazi.
Ikishambuliwa kwa ndani husababisha mirija
kuziba na ikiwa nje ya mirija husababisha
mirija kujikunja.

Matatizo ya kuziba mirija hutokea pale
mwanamke anapopata maambukizi ya mara
kwa mara ukeni yanayoambana na
muwasho kutokwa na uchafu na usaha
ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa na
kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
Maambukizi haya yasipotibiwa kikamilifu
husambaa hadi katika mfuko wa uzazi na
kushambulia tabaka la ndani la kizazi na
kusababisha tatizo liitwalo ‘Endometriosis’
ambapo mwanamke hulalamika maumivu ya
chini ya tumbo au chini ya kitovu mara kwa
mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili
nyingine tulizozielezea hapo awali.

Maambukzi toka ndani ya kizazi husambaa
hadi katika mirija au chini ya kitovu mara kwa
mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili
nyingine tulizozielezea hapo chini.
Maambukizi toka ndani ya kizazi husambaa
hadi katika mirija ambapo hushambulia mrija
mmoja au yote miwili, hapo mgonjwa
huendelea kulalamika maumivu chini ya
tumbo au yanaweza kuwa yamekwisha lakini
maambukizi yaliyojipenyeza huweza
kutafuna mirija na kuziba au kusababisha
usaha, maji na kuvimba.

Maambukizi yanaweza kutokea nje ya kizazi
na mirija na kusababisha mirija ijikunje na
kuziba kabisa hali iitwayo ‘Adhesions’.
Maambukizi yanayoanzia ndani ya kizazi
chanzo chake ni utoaji wa mimba au mimba
kuharibika.
Mirija inaweza kuziba ambapo itakatwa kwa
lengo la kufunga uzazi, inaweza kuziba kwa
bahati mbaya wakati wa upasuaji wa
kuondoa uvimbe kwenye kizazi.
Upasuaji wa mirija kwa lengo la kuzibua pia
inaweza kuongeza tatizo kwani itatengeneza
makovu ambapo mirija itaziba tena.
Maambukizi ya muda mrefu ukeni au katika
mfumo wa uzazi huathiri mirija ya uzazi.

Dalili za kuziba mirija

Mwanamke anayedhaniwa mirija imeziba
anakuwa na historia ya kutafuta ujauzito kwa
zaidi ya mwaka mmoja bila mafanikio.Historia
hiyo inahusiana na kuwa na historia ya
kusumbuliwa na maumivu ya chini ya tumbo
kwa muda mrefu iwe yameshatibiwa au la.
Wengine wanakuwa na historia ya kuzaa
angalau mtoto mmoja au zaidi lakini
anatafuta mwingine anashindwa kupata.
Mwingine ana historia ya kufanyiwa upasuaji
wa tumbo.

Wengi wenye tatizo hili wana historia ya
kuharibikiwa na mimba au kutoa mimba hata
moja tu inaweza kukuzibia mirija yako ya
uzazi. Endapo mrija mmoja utazibika kabisa
basi unaweza kuzaa hata watoto zaidi ya
mmoja kwa kutumia mrija mmoja.

Nini cha kufanya?

Tatizo la kuziba kwa mirija linathibitishwa
hospitali ambapo kipimo kinachoitwa ‘HGS’
hufanyika ili kuthibitisha. Kipimo hiki ndicho
kinachoonyesha kwa usahihi jinsi mrija
ulivyoziba, upo uzibaji ambao mrija baadaye
unaweza kurekebishwa na mwanamke
akapata ujauzito. Picha nzuri ndiyo
itakayomuelekeza daktari jinsi ya
kuurekebisha mrija.
Mrija ukiziba nusu yaani ukiachia nafasi
kidogo kama hautarekebishwa basi kuna
hatari ya kupata mimba na ikabakia kukua
kwenye mrija na hatima yake ni mrija
kupasuka na kuupoteza.

Muone daktari wa magonjwa ya kinamama
na matatizo ya uzazi katika hospitali ya mkoa
kwa uchunguzi na tiba utafanikiwa.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved