Maafisa wa upelelezi kutoka kituo cha polisi cha
Marereni kaunti ndogo ya Magarini
wamewakamata wanafunzi wa Madrassa 36
ambapo waliwahoji kwa takribani muda wa saa
tano kisha kuwaachilia huru.
Vijana hao waliokuwa wametoka katika sherehe
za maulidi huko Mambrui, wamekamatwa katika
kizuizi cha barabara cha Kanagoni baada ya polisi
kupashwa habari.
Wanafunzi hao wa Madrastul Ikhlas Firqatu
Muhibin kutoka eneo la Mvita pamoja na walimu
wao wawili, usiku walihudhuria hafla ya maulidi
katika eneo la Mambrui na alfajiri walikuwa wako
safarini kwenda Lamu wakiwa na basi la shule
walilolikodisha.
Mudiri wa madrasa hiyo Ustadh Shaffy Yahya
amezungumza na kueleza kuwa wamehojiwa kwa
siku nzima na maafisa wa polisi na kuwachiliwa
mwendo wa saa kumi na moja jioni.
Inaripotiwa kuwa maafisa wa usalama walikuwa
wamepata taarifa kutoka Mombasa kuwa basi hilo
lilikuwa limebeba watu hatari kwa usalama.
Ustadh Shaffy ameeleza kuwa wanafunzi wote
wako salama.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Marereni William
Oyugi amesema wanafunzi hao walikuwa wa kati
ya umri wa miaka 20 na 35 na baada ya kuhojiwa
waliruhusiwa kuendelea na safari yao.
Chapisha Maoni