Vipimo
Mchangnyiko wa maharage yaliyochemshwa 2 Vikombe
Nyanya 1 kubwa
Pilipili boga ½
Kitunguu maji chekundu 1
Celery 1 mche (stick)
Parsley (aina ya kotmiri) 1 msongo (bunch)
Mtindi (yoghurt) 1 ½ kikombe cha chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Maji ½ kikombe
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha
1. Katika bakuli, tia mtindi, changanya vizuri na maji na chumvi.
2. Tia thomu uliyosaga.
3. Katakata nyanya, pilipili boga, kitunguu maji, celery na parsely, vipande vidogodogo.
4. Tia mchanganyiko wa maharage
5. Nyunyizia jiyrah (cummin powder)
6. Tayari kuliwa na mikate ya pita au wali wa mboga.
Kidokezo:
Ukipenda unaweza kukatia pilipili mbichi vipande vidogo au sagia pamoja na thomu.
Chapisha Maoni