Vipimo:
Unga mweupe 1 ½ kikombe
Siagi 10 vijiko vya supu
Sukari ya brown (soft brown sugar) ½ kikombe
Baking powder 1 ¾ kijiko cha chai
Mayai 2
Maziwa ¼ kikombe
Walnut zilokatwakatwa (chopped) 1 kikombe
Mdalasini wa unga 1 kijiko cha chai
Chumvi ¼ kijiko cha chai
Vanilla ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Weka siagi nje iwe laini (katika room temperature)
- Washa jiko la oveni kiasi cha 350°
- Weka siagi katika bakuli ipige hadi iwe laini.
- Tia mayai uendelee kupiga
- Tia vitu vikavu vyote .
- Tia maziwa kisha walnuts
- Paka siagi katika treya ya kupikia keki iwe size ya kiasi inchi 8 au 9
- Mimina mchanganyiko wa keki
Chapisha Maoni