WAFUGAJI WAFUNGA MINADA YA MIFUGO MKOANI MOROGORO

0 coment

Wafugaji jamii ya wamasai na wabarabaigi mkoani
Morogoro wamefunga minada yote ya kuuza
mifugo mkoani Morogoro kwa muda usiojulikana
wakilalamikia serikali kushindwa
kukomesha vitendo vya uonevu wanavyofanyiwa
na madereva wa bodaboda.

na madereva wa bodaboda kwa kupigwa na
kufukuzwa kila wanapongia katika mji wa
morogoro.
Wakizungumza kwenye mkutano uliojumuisha
wafugaji kutoka wilaya za Morogoro, Gairo
Mvomero na Kilosa wakiwa na viongozi wao
wakuu wa jadi wanaofahamika kama
malaigwenani wafugaji hao wameazimia kufunga
minada yote kwa muda usiojulikana.
Mbali na maamuzi hayo wafugaji hao pia
wameazimia kuacha kuuza maziwa na
mifugo mkoani Morogoro na watakaobainika
kukiuka agizo hilo watalipishwa faini ya shilingi
milioni moja hadi hapo serikali itapoamua kuingilia
kati migogoro ya wakulima na wafugaji.
Katika hatua nyingine kamati ya ulinzi na usalama
ya mkoa wa Morogoro imetembelea kijiji cha
Mabwegele kujionea athari za watu kuchomewa
nyumba ambapo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt
Rajab Rutengwe amesema serikali haitasita
kuchukua hatua kwa waliohusika na tukio hilo, na
tayari wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya
makazi imemteua Bw Paul Kimiti kufika mkoani
hapa kufanya usuluhishi kwa lengo la kumaliza
migogoro hiyo.
Photo: WAFUGAJI WAFUNGA MINADA YA MIFUGO MKOANI MOROGORO

Share this article :

Chapisha Maoni

Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved