Serikali wilayani mkinga imepiga marufuku
wakulima kusafirisha zao la korosho kwenda nchi
jirani ya kenya bila kuwa na kibali cha bodi ya
korosho nchini tawi la tanga kwa lengo la
kukwepa ushuru na badala yake watumie
utaratibu uliowekwa na serikali wa stakabadhi
ghalani ambao utawanufaisha wakulima na kuuza
bidhaa hiyo kwa tija.
Akizungumza na wakulima wa zao hilo katika
uzinduzi wa kuuza na kununua korosho kwa
mnada ulioanishwa na serikali na kuzinduliwa
katika kata ya duga maforoni,mkuu wa wilaya ya
mkinga Bibi Mboni Mgaza amewashauri wakulima
kukataa mbinu zinazofanywa na baadhi ya
wafanyabiashara kutoka maeneo mbali mbali
kwenda vijijjini kuwarubuni ili waweze kuwauzia
kwa bei isiyokuwa na tija.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima
wameiomba serikali kuelekeza nguvu zake kwa
kuwapelekea pembejeo za kilimo pamoja na
maafisa ugani ili kuliza zao hilo kwa tija huku
baadhi ya wafanyabiashara wa zao la korosho
waliochaguliwa na serikali chini ya mfumo wa
stakabadhi ghalani ambao husafirisha kupeleka
katika masoko ya kimataifa katika nchi za ASIA
wakilalamikia kuwa bidhaa hiyo inapaswa kuwa
na ubora kwa sababu kuna ushindani mkubwa
baina ya nchi za afrika hatua ambayo inaweza
kuharibu sifa ya zao hilo kwa nchi nzima .
Chapisha Maoni