SHERIA ZA KUHALALISHA USHOGA NCHINI KENYA ZAANDALIWA

0 coment



Mjadala mkali unatarajiwa nchini Kenya kuhusu
sheria ambazo huenda zikahalalisha ushoga na
umalaya.
Kulingana na pendekezo la kanuni ya afya
lililofadhiliwa kutoka Marekani, kanuni hizo
zinanuia kuondoa vikwazo vya kisheria
vinavyowazuia watu wa aina hiyo kuwa na haki za
kimsingi kulingana na katiba kwa sababu ya tabia
zao.
Zaidi kanuni hizo pia zitawalinda watumizi wa dawa
za kulevya.
Pia mapendekezo hayo yanataka makundi hayo
kujumuishwa katika bodi mbali mbali za serikali za
kaunti za serikali kuu.

Pia wanataka kuundwa kwa mamlaka
itakayokuwa ikiwashughulikia mambo yao. Kanuni
hizo zinazopendekewa zimetumwa kwa wizara ya
afya.
Mapendekezo hayo yanaeleza kwamba itakuwa
makosa kwa polisi kuwanasa malaya, mashoga na
watumizi wa dawa za kulevya kwa sababu tu
wanafanya shughuli hizo.
Katika taarifa iliyochapishwa katika gazeti la
Standard, shughuli ya kupitia sheria hizo ilikamilika
mwezi Novemba na ilihusisha makundi na
miungano ya wasagaji, mashoga na malaya na
mataifa jirani.

Nchi za Ulaya zimekuwa zikishinikiza nchi za Afrika
kutambua haki za mashoga kwa kuzitishia
kuzinyima misaada endapo hazitatambua haki za
jamii hiyo.
Nchi ya Uganda imeingia katika msukosuko wa
kupunguziwa misaada baada ya kuweka sheria
kali dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya
kishoga.

Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved