Hali ya taharuki imetanda eneo bunge la Mvita
kaunti ya Mombasa siku ya Jumapili baada ya
milio ya risasi kusikika takriban saa tano na
nusu mwendo wa asubuhi.
Mtu mmoja aripotiwa kufariki baada ya
kupigwa risasi kutoka kwa nyuma.
Akithibitisha tukio hilo, mkuu wa Idara ya
Upelelezi mjini Mombasa Henry Ondiek,alisema
mwendazake alivamiwa alipokuwa akiingia
mlango wa Kanisa la Maximum Revival lilioko
eneo bunge la Mvita.
Haijabainika mpaka sasa sababu ya mauaji
hayo huku polisi wakianzisha uchunguzi.
Kufikia sasa, hakuna ishara yeyote
kuonyesha shambulizi hilo lilikuwa ni la
kikabila au kidini.
Bw. Ondiek alisema kulikuwa na maafisa wa
polisi waliokuwa wamesimama lango la pili la
kanisa hilo ambao walimfyetulia risasi
mshambulizi huyo.
Jamaa huyo adaiwa kutoweka kwa miguu na
kupotelea kwenye vichochoro vyembamba
vya mtaa huo.

Chapisha Maoni