Sambaza Habari Hii...
Simu za kisasa zimerahisisha mambo na
kuufanya ulimwengu kuwa mdogo.I
mekuwa kawaida kuona mtu akivuka
barabara na huku anapapasa skrini ya simu
yake katika hali ya kujibu au kusoma jumbe,
kutumia mitandao ya kijamii na kusoma
habari.
Katika utafiti mpya uliochapishwa kwenye
tovuti ya Current Biology, mwanasayansi wa
ubongo Arko Ghosh wa Chuo Kikuu Cha
Zurich aliandika kwamba simu za kisasa
hubadilisha umbile la sehemu za ubongo
zinazotumika kuendesha vidole.
“Simu za kisasa zinatoa fursa ya kuelewa jinsi
maisha ya kawaida yanavyoathiri umbile la
ubongo wa mtu wa kawaida,” aliandika.
Kila kiungo cha mwanaadamu kinamilikiwa
na sehemu yake kwenye ubongo. Sehemu
hizo za ubongo huweza zikabadilika
kulingana na matumizi yake. Kwa mfano,
sehemu ambayo inatumika kuendesha vidole
huwa ni kubwa kwa wachezaji fidla kwa
sababu huitumia sehemu hio mno.
Katika utafiti wake, Ghosh alitumia watu 37,
wenye kutumia mkono wa kulia,aliowapima
chemichemi zao za umeme kwenye mabongo
yao. 26 walitumia skrini za kugusa huku 11
wakitumia simu za kubonyeza.
Aligundua kwamba mabongo ya waliotumia
skrini za kugusa zilikuwa na mabadiliko zaidi.
Pia, aligundua wale walio tumia simu zaidi
ndio waliokuwa na mabadiliko zaidi kwenye
mabongo yao.
Utafiti huo ulidhihirisha kuwa watumizi wa
simu za kisasa wanatumia sehemu ya bongo
inayotawala vidole vya gumba. Pia kulikuwa
na mabadiliko zaidi kwenye kidole cha
kwanza na cha katikati.
Hata hivyo, Ghosh amesema utafiti wake
haujathibitisha vipi mabadiliko hayo kwenye
ubongo yanaathiri maisha ya wanaotumia
simu za kisasa lakini alieleza kwamba
ugunduzi wake huenda ukapelekea utafiti
zaidi kuhusu vipi akili zetu hufanya kazi
katika kuchambua habari.
Chapisha Maoni