ABUU HAMZA |
Mahakama moja iliyoko nchini Marekani
imemhukumu kifungo cha Maisha Da'aia Maarufu
wa Kiislamu Sheikh Mustafa Kamel Mustafa ﻣﺼﻄﻔﻰ
ﻛﺎﻣﻞ ﻣﺼﻄﻔﻰ maarufu kama Abuu Hamza Al
Masri ﺃﺑﻮ ﺣﻤﺰﺓ ﺍﻟﻤﺼﺮﻱ kwa kesi ya kuunga mkono
'Ugaidi'.
Mwendesha Mashtaka wa Marekani amesema
Tuhuma zote 12 aliyotuhumiwa Sheikh Abuu
Hamza Al Masri zimethibitishwa.
Moja ya tuhuma hizo ni kutoa pesa kwa kundi la Al
Qaida na kuhusika kwake na mashambulio
yaliowalenga watalii wa mataifa ya Magharibi
yaliofanyika mwaka 1998 nchini Yemen.
Katherine Forrest ambaye alikuwa Jaji wa kesi hiyo
amemhukumu kutumikia jela miaka 100 Sheikh
Abuu Hamza.
Abuu Hamza ambae ni Mlemavu wa mikono
hukumu hiyo inamaanisha Serikali ya Marekani
imemhukumu Sheikh Abuu Hamza kwenda Jela
Maisha.
Sheikh Abuu Hamza mwenye umri wa miaka 56 ni
mzaliwa wa Misri mwenye uraia wa Uingereza.
Chapisha Maoni