CHADEMA WAMTAKA MAGUFULI ASIWABAGUE WANANCHI CHATO

0 coment

MAGUFULI
Chadema wamtaka Magufuli
asiwabague wananchi Chato

Dk. John Magufuli
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kimemtaka Mbunge wa Chato (CCM), Dk. John
Magufuli (pichani), kuacha kuwabagua wananchi
wa jimbo hilo kutokana na kuwachagua
wenyeweviti na wajumbe wa Chadema kupitia
Ukawa katika uchaguzi wa serikali za mitaa
uliofanyika Desemba 14, mwaka jana.
Chadema walitoa tahadhari hiyo baada ya Dk.
Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, hivi
karibuni kudai atapeleka fedha za Mfuko wa Jimbo
katika vijiji na vitongoji walivyoshinda wagombea
wa CCM pekee.
Katibu Mwenezi wa Chadema wilayani hapa, Alex
Mukama, alisema kutokana na kauli hiyo ya Dk.
Magufuli, inaonyesha wazi jinsi asivyofaa
kuendelea kuaminiwa na wananchi kwa kuwa
anapingana kwa makusudi na Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa
Tanzania inayomtaka kiongozi kujiepusha na
ubaguzi wa rangi, itikadi za kisiasa, kidini na
kijinsia.
Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani ya Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Crispin Kagoma,
aliwashukuru wananchi hao kwa kudhihirisha
wameichoka CCM.
Katika hatua nyingine, Chadema imewaonya
wenyeviti wa vijiji na vitongoji kupitia chama hicho
kutokubaliana na maamuzi ya serikali ya
kuwasumbua wananchi kwa michango ambayo
haijapitia kwenye mikutano mikuu ya vijiji na
kudhaminiwa na wananchi wenyewe.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mkuyuni, Anacret
Lwegoshora (Chadema), alisema baadhi ya
viongozi wa serikali kwa kushirikiana na viongozi
wa CCM, wamekuwa wakiwashinikiza wananchi
kuchangia michango pasipo kuwashirikisha.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved