Miongoni
mwa tofauti kubwa ya Uislamu na imani nyengine ni kuweka muongozo wa
kila kitu katika dira la Kiislamu lililo kamili na lenye kwenda pamoja
na maumbile ya mwanaadamu.
Hutakuta
jambo ambalo ni la msingi, Uislamu ukawa umeacha kutoa tamko lake.
Uchumi, siasa, jamii; vyote vinaangukia ndani ya mwenendo mzima wa
Uislamu. Ni kusema kwamba, Uislamu upo kamili usiotaka kujifunza katika
mambo yasiyo maana kutoka kwenye imani nyenginezo!
Baadhi ya mambo ambayo Waislamu wamegubikwa nayo sana
katika jinamizi la ujinga ni kivazi. Wengi hawaelewi kivazi
anachotakiwa kukivaa Muislamu. Inafika wakati Muislamu anataka fatwa
(jibu) ya kivazi cha kidani kwa mwanamme?? Ni suala ambalo linamuacha
mdomo wazi Muislamu anayeelewa mafundisho ya Uislamu kwamba ni haramu
kuchanganya kivazi baina ya mwanamme na mwanamke.
Tuingie
katika mada yetu ambayo ni maandishi kwenye kivazi cha Muislamu. Ni
sikitiko na pigo kubwa kwa jamii ya Kiislamu kutotilia mkazo kile
kinachovaliwa katika mwili wa Muislamu. Fulana za aina wa aina
zinavaliwa tu bila ya kufuata msingi wa Uislamu. Alimuradi fulana
imependeza mbele ya macho yake na ikawa inaenda na wakati, basi hilo ndio chaguo lake.
Basi
tambuwa kwamba CARLSBERG ni pombe na kila mwenye kuitangaza anatakiwa
kujitayarishia jibu mbele ya Hisabu. Pia elewa kwamba NIKE ni mungu wa
kike wa Kigiriki na kila mwenye kuvaa anaridhia kumshirikisha Allaah
(Subhaanahu wa Ta’ala). Fahamu pia kwamba JESUS ni yule wanayemuitakidi
Manaswara kwamba ni mtoto wa Mungu na kila mwenye kuvaa kinachotokana
nacho anaenda sambamba na Unaswara. Kubali kwamba SOS linasimama kwa maana ya Sword Of the Spirit (Upanga Wa Roho) [Ephesians/Waefeso, 6:17]. Na kila kinachowafikiana na BIBLIA, kwa mfano maandiko yake kwenye fulana basi yawajibika kuepukwa.
Wapo
baadhi ya ndugu zetu wanafikia kuvaa fulana za matusi na inakuwa ni
karaha mbele ya kadamnasi za watu. Yawezekana haelewi maana yake, lakini
dhimma bado inabaki na kwanini asiulize kabla ya kuivaa?!
Halikadhalika
wapo baadhi ya Waislamu wanaopoteza fedha zao kwa kununua kivazi cha
timu fulani. Mwenendo mzima wa maisha yake unakuwa umejaa maandiko ya
timu hiyo, kuanzia taulo, vitambaa vya gari, fulana, suruali na hata
nguo za ndani! Ukoloni huu unaenezwa pia kwa kuwavalisha watoto
wasiotambuwa hata kutamka 'mama' nembo ama jina la timu anayoishabikia.
Iwapo
Waislamu hawaelewei - Nembo za timu za mpira: Timu za Taifa za
Uingereza na zile za Scandinavia zote jezi zao zina Msalaba, LIVERPOOL
ina alama ya msalaba na isitoshe matangazo ya pombe, dragon na picha ya moto, MANCHESTER ina picha ya dragon, ARSENAL ina alama ya bomu lenye duara la tundu sita, na isitoshe wana baadhi ya hisa na Mayahudi, CHELSEA ina picha ya dragon na duara la ua lenye tundu sita. Basi tambua kwamba picha ya dragon, moto, msalaba, duara na mfano wa hayo ni miongoni mwa alama za Umasoni!
Kinamama
nao wanatengenezewa Hijaab zenye nembo za mashirika ya Mayahudi - CK
(Calvin Klein) - na wao wanajiona wamevaa brand na wanakwenda na wakati!
Ni
jukumu la kila Muislamu kuachana na vivazi vya kijahili na pia
kumuamrisha mwenziwe kuachana na kivazi kinachoenda kinyume na Uislamu,
na kwetu sisi hilo tumelifikisha.
Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza, na Utupe rehema itokayo Kwako; hakika Wewe ndiwe Mpaji mkuu.
HII SIO SA HII |
HII NDIO SAHII |
Chapisha Maoni