0 coment

MWENYEKITI MPYA AREJESHA JINA ASILI
LA MASJID MUSA, BADALA YA MASJID
SHUHADAA

MSIKITI katika mtaa wa Majengo, Mombasa, Masjid
Shuhadaa Ijumaa ulirudia jina lake la awali la
Masjid Musa.
Msikiti huo unaoandamwa na serikali ya Kenya,
wakati ukiongozwa na Sheikh Abubakar Sharrif al
maarufu Makaburi ulibadilishwa jina hilo na kuuita
Masjid Shuhadaa mnamo Machi 7, 2014.
Akizungumza na wanahabari Ijumaa, mwenyekiti
mpya wa msikiti huo, Bw Khatib Khamis alisema
waliamua kurudisha jina hilo la awali baada ya
kushauriana na waumini wa hapo.
“Tokea Novemba 27, tulipochukua msikiti huu
kutoka mikononi mwa serikali tumekua
tukiendelea na ibada zetu kwa uzuri, hivyo basi
natoa mwito kwa waumini wenzangu waje
kutuunga katika ibada kwani hali ni shwari
Majengo,” alisema Bw Khatib.
Alihimiza masheikh na viongozi wengine wa kidini
kutoogopa kuhudhuria katika msikiti huo bali
wafike ili waungane kuwezesha kuweka hali iwe
shwari msikitini humo.
Bw Khatib alisema tangia utotoni mwake akiwa
kijana msikiti huo ulijulikana kwa jina la Msikiti
Musa, “Jina hili ni lazima lihifadhiwe, vijana
waliokuja kubadilisha jina hilo hawakumshauri
yoyote na ndio maana wakauharibu msikiti huu,
tunataka jina zuri tulihifadhi ambalo lilikuwa
limepotezwa", alisema.
Alisema toka mwezi wa Novemba, waumini
wamekua wakiongezeka pole pole hivyo basi
anaishukuru serikali ya kaunti na ya kitaifa kwa
kuhakikisha waliupata msikiti huo kwa njia nzuri.
Marehemu Makaburi alitangaza kubadilishwa kwa
msikiti huo kabla ya kuuliwa mnamo Aprili 1, 2014
nje ya korti ya Shanzu.
Alisema kubadilishwa kwa jina hilo ni kuwatukuza
viongozi wa Kiislamu waliouliwa kinyama (Sheikh
Shaaban, Sheikh Sameer Khan na Sheikh Aboud
Rogo) ambao inaaminika waliuliwa na polisi.
Photo: MWENYEKITI MPYA AREJESHA JINA ASILI

LIKE OUR FACEBOOK PAGE CLIK HERE
Share this article :

Chapisha Maoni

Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved