Wakazi wa Mtaa wa Kiangu Manispaa ya Mtwara
Mikindani wakipita kwenye maji kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha mkoani humo. Kwa ufupi
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilaman Ndile
amemwambia mkuu huyo wa mkoa alipotembelea
maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo kuwa
zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika
mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo. Mtwara. Zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji
katika Manispaa ya Mtwara Mikindani kufuatia
mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha
hasara kubwa ambayo thamani yake bado
haijajulikana.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu ametoa saa 24 kwa wataalam
kuhakikisha wanayaondoa maji ndani ya makazi
ya watu.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilaman Ndile
amemwambia mkuu huyo wa mkoa alipotembelea
maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo kuwa zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika
mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo.
Alisema kuwa hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza
maisha kutokana na mafuriko hayo lakini
kumetokea uharibifu mkubwa wa mali na vyakula.
“Mvua kubwa zilizonyesha jana usiku zimeshababisha mafuriko haya…tatizo kubwa mji
wetu hauna mifereji ya kupeleka maji baharini…
athari ni kubwa sana,” alisema Ndile.
Aliongeza kuwa “Mitaa ya Magomeni, Chuno,
Kiangu, Skoya,Kisutu Nabwada ndiyo
yaliyoathiriwa zaidi na tatizo hili” Alia Mussa ni mmoja wa waathirika wa mafuriko
hayo kutoka Mtaa wa Kisutu eneo la Nabwada
alisema kuwa amepoteza fedha kiasi cha
Sh300,000, nguo, chakula na vyombo vya ndani.
“Tunaomba msaada kwa viongozi kunusuru hali
hii, tunaona serikali yetu kama imetutupa, hatuna chakula, wala fedha za kununua chakula, kila kitu
kimeloa,” alisema Mussa.
Dendegu amewaagiza wataalam wa mipango miji,
zimamoto na manispaa kuhakikisha ndani ya saa
24 wanayaondoa maji hayo katika ya makazi ya
watu.
Chapisha Maoni