Kunywa maji safi na salama kwa kiasi kinachostahili kiafya kunaweza
kuyaboresha maisha yako na kukufanya ujihisi mwenye afya na furaha zaidi
.
Kunywa maji ya kutosha kuna faida nyingi. Tukichukulia kunywa maji ya
kutosha ni mithili biashara kati ya wewe na afya yako, biashara hii
inalipa.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji ya kutosha .
-
kusaidia mmeng'enyo wa chakula.
Vimengenya na Kemikali mbalimbali zinazohusika na mmen'genyo au
usagaji wa chakula mwilini ziko katika hali ya mchanganyiko na maji. Ili
hivi viweze kufanya kazi vizuri inatakiwa kuwe na uwiano sahihi kati
yake na maji.Pia maji yanahusika katika kulainisha baadhi ya vyakula .
Pia kunywa maji ya kutosha kunaongeza ufanisi wa mwili katika kusharabu chakula.
-
Dawa ya maumivu ya kichwa.
Mara nyingine maumivu ya kichwa yanasababishwa na upungufu wa maji
mwilini. Hii inamaanisha, kama una maumivu ya kichwa yanayosababishwa na
upungufu wa maji mwilini unaweza kughairi kumeza vidonge vya kutuliza
maumivu na kunywa maji. Hii inawezekana kwenye baadhi ya maumivu ya
mgongo pia.
Pendezesha ngozi yako kwa kunywa maji ya kutosha.
Unaweza kuboresha sura na mguso wa ngozi yako kwa kunywa maji ya
kutosha kwani maji yanasaidia kuboresha tishu za ngozi na kuongeza
unyevu kwenye ngozi .
Maji yanauweka ubongo katika hali nzuri zaidi na ya ufanisi zaidi.
Kunywa maji ya kutosha kunamwezesha mtu kufikiria kwa ufanisi zaidi.
-
kutatua tatizo la kukaukiwa haja kubwa (constipation)
Sehemu kikubwa ya haja kubwa ni maji. Kunywa maji ya kutosha kunaweza
kukusaidia kupata haja kubwa kiulaini na mara kwa nyingi zaidi.
-
kuboresha hali ya viungo na misuli
Maji ya kutosha yanasaidia kupunguza tatizo la kubanwa misuli na pia hupunguza msuguano katika viungo vyako.
Maji yanachochea shughuli za kimetaboliki mwilini na kuongeza ufanisi wa ubongo kwa hiyo yanapunguza uchovu.
-
kupunguza uwezekano wa kupata baadhi ya magonjwa.
Uwezekano wa kupata mafua,mawe ya figo,matatizo ya ini,baadhi ya saratani n.k unaweza kupunguzwa kwa kunywa maji ya kutosha .
-
Maji yanaweza kusaidia katika kupunguza uzito.
Kama uko katika mkakati wa kupunguza uzito maji yanaweza kukusaidia
kwa kiasi kikubwa. Maji huongeza kasi ya shughuli za kimetaboliki
mwilini. Ongezeko hilo la kimetaboliki husababisha mwili kutumia nishati
nyingi zaidi na hivyo huweza kupunguza kiasi cha nishati ambacho
kitahifadhiwa mwilini katika hali ya mafuta au kupunguza kiasi cha
nishati kilichohifadhiwa mwilini.Pia ongezeko la ufanisi wa figo na ini
kutokana na kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa mazao ya mafuta ya
ziada mwilini.
Maji hayaongezi nishati mwilini, kwa hiyo unywapo maji badala ya
juisi,soda au vyakula au vinywaji vingine ambavyo huongeza nishati au
mafuta mwilini unaongeza uwezekano wa kupungua uzito.
"Usinisingizie.Sijasema ushindie maji asubuhi mpaka jioni."
kunywa maji ya kutosha kutakufanya ujisikie vizuri na pia kunaweza
kupunguza safari za hospitali. Kunywa maji ya kutosha, fanya siku yako
iwe poa zaidi.
Chapisha Maoni