1. Jali pesa yoyote uipatayo, usidharau hata
shilingi mia yako maana ukiweza kutunza fedha
ndogo hata kubwa utafanikiwa kuitunza
2. Jenga mazoea ya kufikiria mawazo tofauti ya
biashara hata kama hujawa na mtaji, ili ukipata
mtaji uanze biashara moja kwa moja
3. Mbali na kuajiriwa pia kuwa na fikira za
kuanzisha biashara ndogo ndogo utakazoweka
mtu kuzisimamia ili siku ukiishia fedha ya kutumia
zile biashara zikusaidie.
4. Hakikisha kila fedha uipatayo unaweka akiba
yake maana unaambiwa 'Haba na haba hujaza
kibaba'
5. Usipende kuwa na matumizi yasiyo na lazima
sana, kama unaona bajeti yako haitoshi kufanya
matumizi ya milioni moja usijilazimishe , fanya yale
matumizi uliyo na uwezo nayo na usiiishi kwa
kumuiga fulani.
6. Changamkia kila fursa unayoipata katika
kufikisha malengo yako, ukipata fursa ya kusoma
nenda, ukipata fursa ya biashara fanya, maana
ukiacha fursa zipite utazijitua baadaye.
7. Ishi vizuri na watu maana watu wakuzungukao
ndio wanaweza kufanya wewe ukafikia malengo
uliyonayo maana kila mtu anapotaka kufanya kitu
atakufikiria wewe ila ukijifanya mjanja nao
watakutosa.

Chapisha Maoni