Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua
mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo
iko katika makundi makuu matatu ambayo:
Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi nyuma,
mzunguko wa kawaida wa siku 28 na
mzunguko mrefu wa siku30-35.
Wanawake wengi mzunguko wao huwa ni
wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo
nitawaongelea zaidi.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi
unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza
kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya
kuona damu ya hedhi ya mwezi unaofuata.
Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15
Oktoba basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.
Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28
siku zake za hatari za kuweza kushika mimba
ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku
ya 12 hadi siku ya 16 kama atafanya ngono
bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya
hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono
siku ya 12 anaweza akapata mimba?Hii ni
kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa
kudumu kwa masaa 24 hadi
48 baada ya kujamiiana hivyo kama
mwanamke atafanya ngono tarehe 12 na yai
likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu
zikiwa hai hivyo zitarutubishwa.
Chapisha Maoni