Mwili wa
binadamu ili uweze kuwa katika afya nzuri, unahitaji kuwa na
virutubisho vya kutosha. Virutubisho hivi tunavipata katika vyakula,
matunda na hata kupitia katika vinywaji mbalimbali tunaweza kupata vitu
muhimu kwa ajili ya afya zetu.
Mpenzi msomaji, leo napenda kukufahamisha au kukukumbusha kuhusu faida zinazotokana na ulaji wa tunda hili maarufu sana, TANGO.
Miongoni mwa faida tunazozipata kwa kula matango ni hizi zifuatazo:
Kwanza
kabisa, ulaji wa matango husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo
huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa
cha maji. Maji haya husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu
mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata
vinywaji.
Pili,
husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na matango kuwa na asili ya
nyuzi nyuzi au, fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza
vitu mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito.
Tatu,
hupunguza (hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia
vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na
vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha
akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa
na hangovers.
Nne,husaidia
katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa,
tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na
ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha
ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha
kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.
Tano,
husaidia kuondoa msongo wa mawazo. Matango yana kiwango kikubwa cha
vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali
ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo
wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.
Sita,
husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha
virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na
vitamini c, husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya
mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.
Saba,
husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango
mdomoni kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao
magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni.
Mpenzi
msomaji, tunakushukuru kwa kuendelea kuwa nasi katika blog hii, tutazidi
kukuletea dondoo mbalimbali za afya na usisite kuwasiliana nasi endapo
utakuwa na maoni au jambo lolote la kutushirikisha juu ya afya zetu.
Chapisha Maoni