JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukran kwa swali lako kuhusu namna ya kuswali Swalaah za Sunnah.
Swalaah za Sunnah zinapendeza kuswaliwa Rakaa mbili mbili. Rakaa hizo mbili unaswali kikamilifu na hata kuifanya ndefu kuliko kawaida haswa zile za Swalaah za usiku. Ama shahada (Tahiyyaatu) unaweza kukamilisha hadi mwisho na du’aa, na hivyo ni bora zaidi.
Lakini pia ukifanya kwa ufupi pia hakuna tatizo maadam utakuwa umetoa shahada na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Na Allaah Anajua zaidi
Chapisha Maoni