FAIDA YA TUNDA LA PARACHICHI - PEA (AVOCADO)

0 coment

Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana
ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna
mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na
tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au
hata maziwa kwa kutengeneza juisi.
TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali
(acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama
amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu
maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia
lina protini ya kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye
parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya
moyo, kiharusi na kansa.
VITAMINI “E” NA B6

Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina
kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile
inayopatikana kutoka kwenye mazao ya
wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko
inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika
kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha
kuwa lina faida kubwa mwilini.
Licha ya vitamini E pia ndani ya parachichi kuna
vitamini B6 na kuna madini ya chuma (Iron) kwa
wingi na madini ya potassium, pamoja na vitamin
B6 na E mlaji anaweza kuletawa nafuu sana kama
alikuwa na matatizo ya stress, matatizo ya uzazi
kama ugumba na jogoo kutopanda mtungi Nguvu
za kiume pia tunda hili linasaidia (impotence) .
FAIDA ZA PARACHICHI
Licha ya binadamu kufaidika na virutubisho vya
tunda hili kuna faida nyingi za parachichi kama vile
majani ya mti wake pamoja na magamba, baadhi ya
watu hutumia kutibu maradhi ya kuharisha.
Majani na magamba hayo hutibu pia tatizo la gesi
tumboni, kutuliza kikohozi pamoja na matatizo ya
ini na kusafisha njia ya mkojo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa dawa za
mitishamba, dawa hii haifai kutumiwa na
wanawake ambao wana mimba kwani wakitumia
inaweza kusababisha kuharibika kwa ujauzito.
HEDHI
Hata hivyo, wataalamu wa tiba mbadala wanasema
dawa hiyo inaweza kuwasaidia sana wanawake
ambao wameshindwa kuona siku zao kwa wakati,
na wakitumia vyema wanaweza kuanza kuona
siku zao .
Aidha, tunda hili linasaidia uyeyushaji wa chakula
tumboni hasa kwa wale wenye matatizo ya
vidonda vya tumbo, kwani parachichi lina
nyuzinyuzi “fiber” ambayo ni muhimu kukinga
kuta za utumbo. Watu wenye maradhi ya anaemia,
diabetes, matatizo ya mfumo wa neva, matatizo ya
mishipa ya moyo hasa wa artery wanashauriwa
kula tunda hili mara nyingi.
Lakini pia tunda hili limethibitishwa na wataalamu
kuwa linapunguza kwa kiwango kikubwa
cholesterol kutoka kwenye damu hasa kwa watu
wanene.
Tunda hili husaidia kulainisha ngozi na kuondoa
mikunjo, hung`arisha na kulainisha nywele na
kuzisaidia kukua pia kuziimarisha na kuzuia
kukatikakatika.
Parachichi unaweza kulila kwa kulimenya au kwa
kulisaga na kutengeneza juisi na kama nilivyoeleza
hapo juu unaweza kuchanganya na matunda
mengine kama tulivyoyataja na hutaharibu
virutubisho vilivyomo badala yake utaongeza
ubora wa juisi yako.
Watoto wadogo pia unaweza kuwapa tunda hili na
wakafaidika na haya tuliyoyaandika.
Parachichi pia huweza kutumika kama siagi kwa
kupaka kwenye mkate au kuchanganya na wali.
Haya wale wanaopenda ngozi zao za mwilini
zisijikunje hata wakiwa watu wazima wadumu kula
tunda hili kila siku katika maisha yao basi ngozi za
mwili wao hazitajikunja hata usoni watakuwa kila
siku vijana hata wakiwa wazee.
"Sema : " Ni nani anayekuruzukuni kutoka
mbinguni (kwa kuleta mvua) na katika ardhi (kwa
kuotesha mimea) au ni nani anayemiliki masikio na
macho? Na nani amtoaye mzima katika mfu na
kumtoa mfu katika mzima? Ni nani atengezaye
mambo yote? "Watasema:" Ni MwenyeziMungu",
basi sema; "Je! Hamuogopi?"
10 - 31 Quran
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved