VYAKULA VINAVYOONDOA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI KWA WANAWAKE.

0 coment

Kila mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na
hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni
maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo.
Lakini wanawake wengi husumbuliwa na
matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati
wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati
ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya
muhusika.
DALILI ZA MATATIZO YA HEDHI
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya
wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye
hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili,
huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa,
hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri.
Hali hii husababishwa na kukosekana kwa
uwiano wa homoni (Homone imbalance) na
hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24
baada ya kuanza hedhi.
MAUMIVU MAKALI YA HEDHI
Wengine hupatwa na maumivu makali sana
wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata
akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au
mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia
inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano
wa homoni mwilini, ambako
kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho
fulani.Wengine hutokwa na damu nyingi
kuliko kawaida au kukaa katika siku za
hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida.
Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia
hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu,
kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na
sababu nyingine za kitabibu.
JUISI YA MBOGA ZIFUATAZO HUTIBU
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza
kuepukana na maumivu ya mara kwa mara
wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya
juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika
matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley),
mboga ya majani ambayo upatikanaji wake
ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina
uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni
hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya
hedhi.Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri
kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na
kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’
ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za
jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na
mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya
kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara
kwa mara.Aidha, juisi hiyo inapochanganywa
na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au
matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango
kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na
ujazo sawa kwa kila aina ya juisi
utakayochanganya. Juisi yenye
mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na
ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke
wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji
kutumia dawa zingine kali za kuzuia
maumivu (pain killers) ambazo huwa na
madhara baadaye.
TANGAWIZI NAYO HUTIBU
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu
matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika
tatizo la maumivu makali na kutokupata
hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi,
kiponde na kiweke kwenye kikombe cha
maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia
sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo,
kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.
UFUTA NAO NI DAWA
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu
za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya
hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha
uchanganye na maji ya moto, kunywa mara
mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa
maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana
wadogo.Ukitumia mara kwa mara kinywaji
hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata
hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji
ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta
zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja
kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa
wanaosumbuliwa na maumivu, hasa
ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.
PAPAI NALO NI DAWA
Mwenyezi Mungu ametuumba na kutupa
mazao mengi ambayo yana uwezo wa
kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo
tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo
linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo
wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo
kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi
usio na maumivu. Papai huwa na manufaa
zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye
tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa
na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa
kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo
halijaiva lakini limekomaa)
Photo: VYAKULA VINAVYOONDOA MAUMIVU
WAKATI WA HEDHI KWA
WANAWAKE.

Share this article :

Chapisha Maoni

Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved