ZIJUE FAIDA 10 ZA TENDE KIAFYA

0 coment



Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, tende
ndiyo tunda linaloliwa kwa wingi, pengine
kuliko tunda lingine. Pamoja na kuwa ni tunda
lenye ladha tamu na nzuri mdomoni,
lakini kisayansi pia limethibitika kusheheni
madini na vitamini lukuki, hivyo kuwa na faida
nyingi kiafya. Katika makala ya leo,
nimekuorodhoshea faida zake 10:

1. Ukila tende mara kwa mara, mwili wako
utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za
kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda
hili maarufu duniani. Katika tende kuna kiasi
kidogo tu cha mafuta (fat) na haina lehemu
(kolestrol).

2. Ukila tende, utajipatia kiasi cha kutosha cha
protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C,
virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi
wa afya ya mwili wako kwa ujumla.

3. Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha
mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo
utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo,
au matatizo ya kupata choo kigumu
kinachosababisha maumivu wakati wa
kujisaidia. Pia ndani ya tende kuna virutubisho
vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini.

4. Ukila tende, mwili utapata nguvu na
kukuondolea uchovu ndani ya nusu saa tu,
kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari
asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’.
Ili kupata faida zaidi za tende,
changanya na maziwa fresh kisha kula.
Unapojisikia mchovu, badala ya kunywa
vinywaji baridi vinavyodai kuongeza nguvu,
kula tende, hata kiasi cha punje tatu kinatosha.
Kwa wafunga saumu, ndiyo maana
inashauriwa kuanza kufungua kwa kula tende
ili kuurejeshea mwili wako nguvu iliyopotea
siku nzima.

5. Tende ina madini pia aina ya ‘potassium’ na
kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini haya
husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu.
Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa
‘potassium’ huweza kumuepusha mtu na
kupatwa na kiharusi (stroke). Pia tende
husaidia kupunguza lehemu (cholesterol)
mwilini (LDL Cholesterol).

6. Kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa
kukauka damu mwilini (anemia), wanaweza
kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi
ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini
ya chuma ambayo huhitajika katika
utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu
vitamu vingine huozesha meno, utamu wa
tende huzuia uozaji wa meno.

7. Kwa tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu
wa choo, loweka tende za kutosha kwenye
maji kiasi cha lita moja usiku kucha, kisha
asubuhi changanya maji hayo pamoja na hizo
tende ili upate juisi nzito, kunywa na choo
kitafunguka na kuwa laini.

8. Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za
kiume, mchanganyiko maalum wa tende,
maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza
kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja
kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya
mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha.
Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa
hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi
cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na
unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo.
Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi
utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.

9. Tende ni dawa ya unene, kwa wale wenye
matatizo ya wembamba wa kupindukia na
wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila
siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana
kwamba, wale wanaohitaji kupunguza uzito,
ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa. Pia
tende husaidia uondoaji wa kilevi mwilini.

10. Tende inatibu saratani ya tumbo. Habari
njema kuhusu tende kama tiba ni kwamba,
haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa
asilia na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za
‘kizungu’. Tende vile vile ina imarisha nuru ya
macho na tatizo la kutokuona usiku (night
blindness).
Kwa ujumla faida za tende ni nyingi na
unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali,
kama vile kuchanganya na maziwa,
kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine.
Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa
kila siku ili ujipatie faida hizi 10 na nyingine.

Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved