UGONJWA WA MAFINDOFINDO (TONSILS)

0 coment


Tonsil husababishwa na sababu nyingi tu .
Pia husababishwa na upungufu wa white
blood Cells katika mwili ambazo cells hizi
ndio hupigana na vidudu vyote venye
kuleta maradhi ndani ya mwili sasa
vinaposhindwa kufanya kazi lymph
zinavimba na husababisha Tonsils.
Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili,
wapo ambao wanapata tonsils kwa
kunywa maji ya baridi ambayo maji ya
baridi huwa ni moja katika chanzo cha
kupata tonsils, mavumbi huchangia vile
vile pilipili na vitu vikali kama vile embe
mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya
kupata tonsil.
Wakati unapokuwa na tonsils muhimu
zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote
vikali, zaidi utumie maji ya moto
Dawa za tonsils ni : kama ni mtumiaji wa
dawa za chemicals basi epincilin inasaidia
sana kuondosha tonsils.
Dawa nyengine ambayo mimi binafsi
naipendelea hii zaidi kwani inafanya kazi
mara moja : Kamua ndimu moja katika
glass yako kisha tia maji ya Uvuguvugu
(warm water) na baadae tia vijiko vinne
vidogo vya asali na kijiko robo cha
chumvi kuroga uzuri na unywe pole pole
Au Dawa hii Jaribu pia Dawa ya TONSILS ni
kusukutuwa maji yaliokuwa si moto sana
pamoja na chumvi mara 4 kwa siku
yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili
pili manga wala Tangawizi. Kwani watu
wengi utasikia wanakunywa chai ya
tangawizi na soup iliyojazwa pili pili
manga. Kumbe unaona vizuri wakati
unapokunywa lakini huwa
unayavimbisha matonsils kwani baada
ya nusu saa utaona unaumwa kuliko
mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa
unakunywa maji ya moto moto.
Vile vile kuchukuwa mdomo wako na
kuweka kwenye goti na kuwa
unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa
mara na kama hufikii goti lako basi
unaweza kuchukuwa kanga na kufanya
mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila
utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia.
Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa
dharura kwani ujaribu utakavyoweza
upepo usipite kwenye mdomo wako.
Sio lazima unywe maji baridi ndio upate
Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo
wa baridi unapita kwenye mdomo wako
basi unapata Tonsils Au wakati unapolala
na A/c linafanya kazi na mdomo uko wazi
basi pia unaweza kuumwa na Tonsils.
Vile vile kutoka nje kwenye joto kisha
ukaingia pahala baridi huwa inasababisha
Tonsils na maradhi mengine kama flu na
kuumwa na kichwa..n.k
Dawa Ya Kienyeji mie naita Five in One.
1) Glasi moja ya maji Safi ya kunywa.
2) Kijiko 1 cha Asali Safi ya nyuki
wakubwa.
3) Kijiko 1 cha Uwatu iliyosagwa (Hilba)
kwa lugha ya kiingereza inaitwa
Fenugreek
4) Tangawizi (fresh)
5) Kipande cha ndimu
kisha zichanganye pamoja halafu
chemsha kama unavyo chemsha chai,
ngojea ipoe moto kidogo kisha unywe
kama unavyo kunywa chai kutwa mara 3
kwa muda wa siku 3 au siku 7.
Share this article :

Chapisha Maoni

 
Designed By AL HUDDAH
Islamic foundation
Copyright © 2013. RIAD BIN RUWEHY | All Rights Reserved