Duka la reja reja la Nakumatt limetangaza
mpango wake wa kufungua matawi 14
mapya kwenye muda wa miaka miwili ijayo.
Mkurugenzi wa Mikakati na Oparesheni wa
kampuni ya Nakumatt Holding, Thiagarajan
Ramamurthy, alisema kuwa mipango ya
kufunguwa matawi 14 nchini Kenya na nchi
za jirani iko karibu kukamilika na ujenzi huo
utaanza karibuni.
Ramamurthy alisema: “Tunaangalia mbele
kwenye kujikuza na hatutababaika na
washindani wapya wanaoingia kwenye soko
katika hali ya kutaka kufurahisha wateja
wetu na kukuza upana wetu.”
Kulingana na Ramamurthy, mpango wa
Nakumatt ni kufikisha mauzo ya Shilingi 90
bilioni hivi karibuni.
Nakumatt walifanya mauzo ya shilingi 56.5
bilioni mwaka 2013 ikiwa ni karibu mara
mbili ya mauzo ya mwaka 2012 ambayo ni
shiligi 29.5 bilioni.
Kufikia sasa, Nakumatt ina matawi 52 kwenye
miji mbali mbali nchini Kenya pamoja na
Uganda, Tanzania na Rwanda.
Mkurugenzi huyo alizungumza alipokuwa
akimzawadi mshindi wa shindano la
Nakumatt la Christmas Bonanza gari aina ya
Ford Figo.
Chapisha Maoni